Baada ya habari nyingi kusambaa kuwa Haji Manara kuondolewa kwenye nafasi yake ya usemaji wa Simba, hatimaye leo kupitia ukurasa wake wa Instagram amedhibitisha kuwa yeye ndiye atakuwa msemaji wa Simba.
Haji Manara ameandika kuwa bodi ya wakurugenzi imemchagua kuwa msemaji mkuu wa Simba huku akishukuru kwa bodi pamoja na mtendaji mkuu mpya wa Simba.
“Asanteni sana Wanasimba wote hususani bodi ya wakurugenzi chini ya mwenyekiti watu Mohammed Dewji lakini kubwa kwa CEO wetu mpya Mr Senzo kwa kuendelea kuniamini kufanya kazi katika klabu hii kama msemaji wao rasmi. InshaAllah nitafanya kazi hapa kwa spirit Ile ile!, done deal. Simba nguvu moja.”