Sambaza....

Tumekuletea habari zinazogonga vichwa vya habari Barani Ulaya kwenye Ligi ya Mabingwa pamoja na usajili wa vilabu vikubwa.

Klabu ya Real Madrid huenda ikafikiria kuachana na winga wake Vinicius Juniour na kumsajili Kylian Mbappe. Vinni mkataba wake utaisha mwishoni mwa msimu ujao huku mazungumzo ya mkataba mpya yakisuasua, huku ikitajwa kushuka kiwango na kupenda kulalamika mno na kuwakera wachezaji wenzake kitu kinachomkera rais wa Madrid Florentine Perez. [El Desmaque]

 

Liverpool bado wapo mstari wa mbele wakitaka saini ya nyota wa Dortimund Jude Bellingham lakini ni lazima wafuzu kwanza Ligi ya Mabingwa msimu ujao ili kuweka hai matumaini yao yakumpata nyota huyo wa England.

Dortmund hawatopunguza ada ya uhamisho ya €150 milioni iliyowekwa kwa Bellingham na hivyo Liverpool bado atapaswa kupambana na Real Madrid wanaomuhitaji pia kiungo huyo. [Football transfers].

Klabu ya Newcastle United imeonyesha nia ya kumhitaji mlinzi wa kati na nahodha wa Manchester United Harry Maguire. Vilabu vingine vya Wolverhamton na West Ham wameonyesha nia yakumuhitaji mlinzi huyo wa kati.

Nyota wa Bayern Munic Thomas Mullar amesema mambo huwa marahisi uwanjani kila wakikutana na Lionel Messi kwenye kupata matokeo. Mulla pia ameongeza huwa wanakua na wakati mgumu zaidi pindi wanapokutana na Cristiano Ronaldo haswa pindi akiwa Real Madrid. [Goal.com]

Manchester United wameonyesha uhitaji wa saini ya kiungo wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa Eduardo Camavinga. United wapo tayari kutoa €130 milioni ili kupata huduma ya nyota huyo aliecheza fainali ya kombe la Dunia. [90 mins]

Joao Cancelo atapaswa kurejea klabu yake ya Manchester City mkopo wake utakapomalizika katika klabu ya Bayern Munich baada ya Bavarians kutotaka kutotaka kutoa €70 kumnunua jumla nyota huyo kutoka Ureno. [Fabrizio Romano]

Sambaza....