Pazia la Ligi Kuu lilifunguliwa siku ya Jumapili iliyopita, mtandao wetu wa Kandanda.co.tz umekuandalia matukio matano ambayo ni vyema ukayaweka katika kumbukumbu zako
Goli la kwanza la Ligi
Bigirimana Blaise kutoka klabu ya Namungo FC ndiye anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli la kwanza katika mechi ya kwanza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom. Bao hilo lilifungwa katika dakika ya 64 dhidi ya Coastal Union FC.
Blaise msimu uliopita aliifungia klabu yake mabao 10
Kipigo kikubwa cha kwanza
Mbeya City FC, msimu uliopita waliponea chupuchupu kushuka daraja, wamefungua pazia kwa kuwa timu ya kwanza kupachikwa mabao mengi zaidi pale ilipocheza na KMC FC katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kadi nyekundu yakwanza
Chona Nurdin, kutoka klabu ya Prisons, ndiye mchezaji wa kwanza kupata kadi nyekundu. Akiendeleza record ya klabu yake ya Prisons katika kupata kadi ya mwanzo nyekundu kwa misimu mitatu mfululizo.
Extraordinary Record
Ni msimu wa 11 sasa wa Kapteni wa Simba SC, John R. Bocco akifunga magoli. Hakika hii ni extraordinary record. Tunastahili kusimama na kumpigia makofi John Bocco. Bofya jina lake kupata taarifa zake.
Kwa misimu mitatu pia klabu yake ya Simba imetwaa ubingwa wa ligi Kuu Tanzania bara, na kufanya vizuri zaidi katika michuano ya kimataifa.
Ligi kuu inaendelea tena mwishoni mwa wiki hii, bofya hapa kujiunga ubashiri michezo ya Kandanda.