Sambaza....

LICHA ya kuanza msimu kwa mwendo wa kuridhisha ikiwemo kuongoza ligi kuu kwa wiki kadhaa, habari za ndani nilizozipata ni kwamba wachezaji wa Mbao FC wameanza kumpa wakati kocha mkuu wa timu hiyo Amri Said ´Stam´.

Jumanne hii Amri aliingia katika mzozo na uongozi wake akiwashinikiza kuwalipa mishahara wachezaji wake baada ya baadhi yao kuanza kufikiria kugoma kufanya mazoezi ama kuondoka klabuni hapo katika usajili huu wa dirisha dogo Tanzania Bara.

Timu hiyo ya Mwanza kwa sasa ipo nafasi ya nane katika msimamo wa ligi ikiwana alama 19 baada ya kucheza michezo 13 inaweza kumpoteza mfungaji wake namba moja Said Khamis anayewaniwa na timu za Kagera Sugar FC, KMC FC.

” Leo (jana) kulikuwa na mzozo kati ya kocha ( Amri) na uongozi wa timu kutokana na mwalimu kupeleka malalamiko kwa uongozi akitaka uwalipe mishahara wachezaji na benchi la ufundi, hali ambayo imeanza kuleta wasiwasi wa timu kuanza kufanya vibaya katika michezo yao ijayo.” Kilisema chanzo cha habari hii kilichoomba ifadhi ya jina lake.

Inasemekana wachezaji na benchi la ufundi wanadai mishahara ya kuanzia September mwaka huu na sasa uvumilivu unaaanza kuwashinda.

Sambaza....