Mtandao wa African News hivi karibuni uliripoti tuhuma nzito ambazo zilimuhusu Rais wa CAF, Ahmad Ahmad na Marais wa shirikisho la Tanzania, Wallace Karia na Cape Verde bwana Victor Osório.
Tuhuma hizo zitolewa na aliyekuwa katibu mkuu wa CAF Amr Fahmy baada ya kutimuliwa siku chache kabla ya upangwaji makundi wa Michuano ya Afrika ambayo inafanyika nchini Misri.
Tovuti yetu imepata nakala ya barua ambayo inaonyesha kwa uwazi kiasi kilicholipwa kwa shirikisho na marais na kwa madhumuni gani. Barua hiyo iliyosainiwa na Amr Fahmy inaonyesha kiasi cha pesa na matumizi yake.
Malipo hayo pia kwa mujibu wa barua hii inaonekana yaliidhinishwa na mkutano mkuu wa CAF chini ya Rais wake Bwana Ahmad Ahmad, katika kikao ambacho Amr ni mjumbe pia.
Malipo ya Msaada kwenda kwa kila mwanachama wa Shirikisho yenye jumla ya dola 100,000 (milioni 230 -1$=2300Tsh):
- 20,000$ (Milioni 46) Malipo ya ziada (Allowace) kwa marasi wa shirikisho
- 50,000$ (Milioni 115) Kwaajili ya kusapoti kandanda la vijana
- 30,000$ (Milioni 69) Kwaajili ya waamuzi
Tuhuma zipi hizo alizoziandika Amr Fahmy juu ya Rais wa CAF na kuripotiwa katika mitandao tofauti na Reuters ikidai kuwa ina nakala za ripoti hiyo ni hizi:
- Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Arais wa Cape Verde wadaiwa kuwa miongoni mwa walionufaika na TZS milioni 46 ($20k) kila mmoja zilizogawiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad zinazodaiwa kuwa ni rushwa.
- Rais Ahmad anatuhumiwa kwa rushwa na matumizi mabaya ya ofisi, ikiwa ni miaka miwili tu tangu alipotwaa uongozi wa chombo hicho kikubwa cha soka Afrika.
- Ahmad Ahmad aliisababishia CAF gharama ya ziada ya takribani TZS bilioni 2 ($830,000) kwa kuagiza vifaa kupitia kampuni ya Ufaransa ijulikanayo kama Tactical Steel.
- Pia anatuhumiwa kuwadhalilisha watumishi wanne wakike wa CAF ambao majina yao hayakuwekwa bayana.
- Zaidi Ahmad Ahmad anatuhumiwa kukiuka sheria za CAF na kuongeza uwakilishi wa Morocco ndani ya shirikisho hilo.
- Aidha anatuhumiwa kutumia zaidi ya TZS milioni 925 ($400,000) of CAF za CAF kwa ajili ya magari nchini Misri na Madagascar ambapo ofisi ndogo za CAF zimefunguliwa.
Nafasi Amr Fahmy ambaye ni raia wa Misri imechukuliwa na Mouad Hajji kutoka Morocco.
Katika tuhuma hizi zote hapo juu bado CAF haijatoa taarifa yake rasmi kuelezea. Ingawa hawakuwa wazi pia sababu iliyofanya Amr afukuzwe kazi siku chache kabla ya upangwaji makundi ya AFCON 2019.
Swala kubwa la kujiuliza na ambayo kandanda inajaribu kufuatilia, je pesa hizi zinafanya au zilifanyiwa kazi kwa mujibu wa madhumuni yake?
Kwa upande wa Tanzania yawezekana ndizo zinazosaidia shirikisho katika uendesheaji wa timu za vijana na mambo mengine, ambayo matunda yake yanaonekana Serengeti Boys pia.