Sambaza....

Shirikisho la Soka Ulimwenguni, FIFA, limempiga faini ya dola za kimarekani 503,169.50 (sawa na bilioni 1.2) Jamal Malinzi, Rais wa zamani TFF,  baada ya kupatikana na hatia ya kutumia vibaya fedha kutoka shirikisho pamoja na ‘kufoji’ nyaraka.
Matumizi hayo mabaya ya fedha yanajumuishwa zile kutoka FIFA, CAF na TFF yenyewe. Pamoja na hilo, amefungiwa miaka 10 kujihusisha na masuala ya mpira wa miguu kwa miaka 10 ndani na nje ya nchi.


Mtandao wa Kandanda, umekusndslia Dondoo zote kutoka katika hukumu ya Fifa.


 

Bw. Jamal Emil Malinzi, Mtanzania, alikuwa Rais wa TFF kati ya mwaka 2013-2017. Malinzi pia alikuwa katika kamati ya ‘Fair Play’na “Social Responsibility’kati ya mwaka 2013-17 pia mjumbe wa kamati ya maendeleo ya Fifa kati ya Januari-Oktoba 2017 #HukumuYaFifaKwaMalinzi

Juni 29, 2017: Malinzi (Rais), Selestine (Katibu) na Bi Mwanga(Akaunti) walifikishwa mahakamani wakishtakiwa na makosa 28 yakiwemo Kufoji nyaraka, malipo na utakatishaji fedha. Malinzi pekee anamshtaka 23.

Malinzi katika makosa 23 alidanganya, akisema amelikopesha shirikikisho (TFF) milioni 454.4, pia kupitia makubaliano ya ripoti ya kamati tendaji ya TFF ya tarehe 5 Juni, 2016 alijipatia dola 375,418 kwa udanganyifu.

Ripoti ya ukaguzi ya FIFA ya Julai 17,2017 ilionyesha uwalakini katika matumizi ya fedha pamoja na ukiukwaji wa taratibu katika kusimamia fedha za miradi zinazokuja TFF.

Disemba 18,2017 Kamati ya  FIFA ilitoa ripoti ya uchunguzi ikitanguliwa na ya kamati ya maadili tarehe 8 Disemba, ilipnyesha mapungufu katika usimamizi wa fedha zinazokuja TFF Kutoka FIFA.

Kutokana na uchunguzi wa awali, Mwenyekiti wa kamati Uchunguzi, Bi Maria Claudia Rojas, waligundua kuwa Bw Malinzi amevunja vifungu vilivyomo katika Maadili ya FIFA. 

April 1,2019 Malinzi alipewa taarifa kuanzwa kwa uchunguzi kumchunguza kuhsu uvunjwaji wa vifungu kutokana na uchunguzi wa awali. Uchunguzi huu uliongozwa na Bi Maria Claudia Rojas

May 14, 2019 upelelezi ulikamilika na kukabidhiwa kwaajili ya maamuzi huko Fifa.

Malinzi alipewa taarifa kutoa tamko lolote, kitu ambacho hakufanya, na alitakiwa kuwepo kujitetea pia hakutokea, hivyo kamati ya Fifa ilifanya uamuzi kwa kutumia ripoti zake. 

Jamal Malinzi anatakiwa alipe Bilioni 1.1 ndani ya siku 30 kuanzia leo.

Atalipia gharama zote za undeshwaji wa kesi yake hii.

Hatajihusisha na mpira wa miguu ulimwenguni kwa kipindi cha miaka 10.

Sambaza....