Zanzibar Heroes imeanza kwa kujivuta michuano ya Challenge nchini Uganda baada ya kufanikiwa kuanza na sare mbele ya Sudan katika mchezo wa kwanza wa Kundi B.
Kikosi cha Zanzibar kikiwa kimesheheni nyota wanaocheza Ligi Kuu Bara wanatakiwa wajialaumu wenyewe kwa kupata sare katika mchezo huo baada ya kuruhu bao katika dakika ya tisini ya mchezo.
Zanzibar Heroes ndio waliokua wakwanza kupata goli baada ya mshambuliaji wake aliengia kutoka benchi Makame Mussa kufunga goli hilo akitumia vyema makosa ya walinzi wa Sudan na kupachika mpira nyavuni katika dakika ya 54.
Sudani walifanikiwa kusawazisha goli katika dakika ya tisini ya mchezo kwa shuti la nje ya kumi na nane baada ya walinzi wa Zanzibar wakiongozwa na Ally Ally kushindwa kuondoa mpira kwenye lango lao.
Zanzibar walijikuta wakimaliza mchezo wakiwa pungufu baada ya mshambuliaji wao Ahmada Amada kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 86.
Kipa wa Zanzibar pia ameonyesha kiwango kizuri katika mchezo huo kwa kuokoa michomo hatari katika lango lake ikiwepo kuokoa mkwaju wa penati katika dakika ya 35 na kuisaidia Zanzibar Heroes kupata walau alama moja.
Kwa matokeo hayo goli la Mussa Makame limeshindwa kuipa alama tatu Zanzibar Heores. Zanzibar sasa wanasubiri kuvaana na ndugu zao Tanzania Bara katika mchezo unaofuata!