Mshambuliaji tegemeo wa klabu ya Yanga, Heritier Makambo, amekiri kuwa yeye mambo yake na Horoya FC yamekamilika na yupo tayari kuondoka.
“Mimi naipenda Yanga sana…Mambo yangu yote na Horoya yameshaisha” Makambo alisema haya wakati akihojiwa na kituo cha luninga cha AZAM mara baada ya mchezo wa Yanga SC 1-0 Mbeya City FC kumalizika.
Katika mchezo huu, makambo ndio alikuwa mfungaji wa bao pekee hilo.
Tazama hapa orodha ya mechi alizofunga magoli yake 17 hadi sasa katika ligi kuu ya Tanzania bara.