Sambaza....

Bado wako katika kampeni za kuusaka ubingwa, kampeni ambazo zinaonekana kwao zinaenda vyema. Mpaka sasa hawajafungwa hata mechi moja.

Wameshinda mechi 10 kati ya mechi 12 ambazo wamecheza msimu huu kwenye ligi kuu Tanzania bara.

Kwanini Yanga wanahitaji mshambuliaji mwingine?

Hii ligi ni ndefu kuna wakati wachezaji hupata majeraha, huchoka kutokana na wingi wa mechi pamoja na safari za mikoani. Kwa hiyo vitu hivi husababisha mchezaji husika kushuka kiwango. Anaposhuka kiwango huitajika mtu ambaye anaweza kusimama kama mbadala wa mchezaji husika baada ya kuumia au kupata uchovu.

Ukitazama benchi la Yanga halina mshambuliaji ambaye anakiwango ambacho kinaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa. Kwa sababu mbadala mkubwa wa Makambo mpaka sasa ni Amis Tambwe ambaye anakumbwa na majeraha ya mara kwa mara pamoja na kiwango chake kushuka.

Kiwango cha Makambo kinatia moyo wa kumwamini kuwa anaweza kusimama kama mshambuliaji pekee wa kutegemewa ndani ya timu ya Yanga?

Hapana, amekuwa mchezaji ambaye anakosa nafasi nyingi sana ndani ya mchezo. Nafasi ambazo kama angekuwa mshambuliaji makini (Clinical Finisher) , Yanga ingekuwa sehemu nzuri.

Ngao ya Jamii

MsimuTimu
Jumla-

TPL

MsimuTimu
2018-2019Yanga SC17000000
Jumla-17000000

Kuwepo na mshambuliaji wa kati wa ziada ambaye anauwezo mkubwa wa kufunga unaipa nafasi kubwa Yanga ya kuwa na njia mbadala kipindi ambapo timu inapobanwa au kipindi ambapo mshambuliaji husika anapokuwa amebanwa.

Kwa hiyo pamoja na Yanga kuonekana inashinda kwenye hizi mechi ambazo wamecheza ugenini (Dhidi ya Mwadui na Kagera Sugar) huku Makambo akifunga kwenye mechi zote mbili, inahitaji mshambuliaji wa ziada ambaye ataongeza nguvu kwenye hizi mbio ndefu za ubingwa. Ligi ni ndefu ina mechi 38 , mpaka sasa Yanga imecheza mechi 12 bado mechi 26. Kwa hiyo inatakiwa ijidhatiti na kikosi imara ambacho kitaisaidia kuchukua ubingwa msimu huu.

Sambaza....