Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzânia “TaifaStars” kitakachocheza na Cape Verde kina mjumuisho wa wachezaji 9 wanaocheza ligi za nje ya Tanzania.
Huenda kwa kipindi hiki kikosi cha timu ya Taifa kikawa na wachezaji wengi wanaocheza soka nje ya nchi! Watatu wakiwa wanatoka Ulaya huku wengine sita wakitokea África. Farid Mussa na Shabani Chilunda (CD Tenerife- Spain), Mbwana Samata (KRC Genk- Belgium), Himid Mao (Petrojet – Misri), Simon Msuva (Diffaa El-Jadida- Morroco), Thomas Ulimwengu (Al Hilal – Sudan), Hassan Kessy (Nkana Red Devil’s – Zambia) na Abdi Banda (Baroka- Africa Kusini).
Lakini katika wachezaji wote 9 ni wachezaji wawili tu ndio wanaocheza nafasi ya ulinzi ambao ni Abdi Banda alie Baroka na Hassan Kessy wa Nkana ya Zambia. Kwa maana hiyo asilimia kubwa ya wachezaji wanaocheza nje wanaounda Taifa Stars wanacheza nafasi ya ushambuliaji na kiungo.
Abdi Banda ndie mchezaji pekee mwenye uzoefu katika soka la kulipwa akiwa nwaka wa pili sasa katika Ligi ya Africa kusini, huku Hassan Kessy akifuata nyayo na kufanya kuwa na wachezaji wawili wa kulipwa katika idara ya ulinzi.
Ili timu iwe na “balance” katika maeneo yote uwanjani ni vyema tukapata pia idadi kubwa ya walinzi wanaocheza soka la kulipwa kama ambavyo tuna idadi kubwa katika eneo la ushambuliaji!
Ukimtazama Abdi Banda “VVD” wa Leo sio yule wa Simba kwa maana kua amebadilika kiuchezaji na kuimarika haswa. Ana utulivu, akili nyingi na maamuzi sahihi wakati wote akiwa analinda ngome yake.
Lakini Abdi Banda pekee hatoshi kuifikisha Taifa Stars pale tunapopataka hivyo basi kama ambavyo Mbwana Samata akiwa na wasaidizi wengi katika eneo la ushambuliaji (Kina Msuva, Ulimwengu na Shabani Chilunda) ndivyo hivyo pia Abdi Banda anahitaji wasaidizi pia katika eneo la ulinzi!
Ni wakati sasa wachezaji wetu wanaocheza nafasi za ulinzi (walinda mlango na mabeki) não wapate uchungu na kusogea mbele ili tupate idadi kubwa pia katika eneo hili.
Japo inawezekana Mbwana Samata alikua chachu ya kua na wachezaji wengi wanaocheza nje katika eneo la ushambuliaji kutokana na mafanikio aliyoyapata. Hivyo basi ni zamu ya Abdi Banda kuwafanya wachezaji wetu wanaocheza eneo la ulinzi kutamani kua kama yeye.
Gadiel Michael, Yusuph Mlipili, Andrew Vicente, KenedKe Juma, Benedict Tinoco na wengine wengi tukeni nje tuwe na kina Abdi Banda wengi tuisadie timu ya Taifa.
Japo mpaka sasa inaonekanaa kwa kiasi kikubwa bado wachezaji wanaocheza nafasi za ushambilliaji kuendelea kupigania nafasi ya kutoka kwenda kwenye soka la kulipwa. Yahya Zaid alikua Africa Kusini kwa majaribio, lakini pia Habibu Kyombo huenda wakati wowote akajiunga na Mamelody Soundown baada ya kufuzu majaribio yake aliyoyafanya mwezi August!