Liverpool wameendeleza dhamira yao ya kuhakikisha wanashinda kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu, baada ya kuichapa As Roma kwa mabao 5-2 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa kunako dimba la Anfield jijini Liverpool, Uingereza
Shujaa wa Liverpool alikuwa ni Mohammed Salah, aliyefunga mara mbili kabla ya kutengeneza mabao mengine mawili na Liverpool kuanza kuchungulia fainali ya michuano hiyo
Roberto Firminho pia amefunga mabao mawili, huku mshambuliaji Msenegali Sadio Mane akifunga bao moja na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga
Hii inakuwa mara ya 8 kwa Sadio Mane, Roberto Firminho na Mohammed Salah wote kufunga katika mchezo mmoja.
Pia mabao mawili aliyofunga Salah yanamfanya kufikisha idadi ya mabao 43, akiwa na Liverpool msimu huu akifukuzia rekodi ya Ian Rush ya msimu wa mwaka 1983/84 ambapo alifunga mabao 47, kwa msimu
Mabao mawili alifunga Firminho anafikisha idadi ya 10, na kuifikia rekodi ya ufungaji wa idadi hiyo katika michezo michache, Adriano alifunga mabao 10 katika michezo 11.
Edin Dzeko na Diego Peroti waliifungia Roma mabao mawili, na kufufua matumaini pengine wanaweza kubadili matokeo katika mchezo wa marejeano utakaofanyika kunako dimba la Estadio Olympico jijini Roma, Italia