WAKALA wa mchezaji Nabil Fekir, amethibitisha kwamba klabu ya Liverpool hakuna walichokifanya mpaka sasa katika mahitaji ya kuwa na mchezaji huyo anayekipiga katika klabu ya Lyon katika Ligi kuu ya Ufaransa
Fekir ambaye alifunga mabao 18 ya ligi katika msimu uliomalizika akiwa na Lyon katika Ligi kuu ya Ufaransa, ambapo ameisaidia klabu yake kumaliza nafasi ya tatu kutoka juu ya mabingwa wa kukimbia Paris Saint-Germain
Aina ya uchezaji kwa mchezaji mwenye umri wa miaka 24 imekuwa ikiwavutia sana Liverpool, na kutamani kuwa nae katika msimu ujao. Lakini bado kwa matamanio hayo klabu hiyo bado haijafanya mazungumzo yoyote pamoja na klabu ambayo ina msimamia Fekir kwa sasa
Wakala huyo anaye tambulika kwa jina la Jean-Pierre Bernes alieleza kwamba, bado anashangaa kuiona Liverpool ikimuhitaji mteja wake pasipo kufanya mazungumzo ya awali na klabu ya Lyon
“Majadiliano na Liverpool yatatokea tu wakati ambapo tayari watakuwa wamefanya makubaliano na Lyon, ili kuonesha mwanga zaidi katika dili hili”
“Nia ya Liverpool ipo lakini kwa sasa hakuna kitu kinachofanyika dirisha la usajili lipo wazi, hivyo vinaweza kutokea vilabu vingine na kuonesha maslahi zaidi,” alifafanua wakala huyo