Sambaza....

Simba sc, imeshindwa kupata ushindi ugenini dhidi ya Lipuli FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1

Katika mchezo huo ulioanza kwa kasi, huku wenyeji wakifaidika na umilliki wa mpira kwa kiasi kikubwa baada ya kufanikiwa kupata bao kunako dakika ya 31, ya kipindi cha kwanza likifungwa na Adam Salamba

Bao hilo, lilidumu kwa kipindi chote cha kwanza ambapo mpaka mwamuzi Hanc Mabena, wa Tanga, anapuliza filimbi kuashiria mapumziko Lipuli walikuwa mbele kwa bao hilo

Kipindi cha pili Simba sc, walionekana kuamka na kuanza kuwashambulia sana wenyeji wao huku kocha Pierre Rechantre akifanya mabadiliko ya kumtoa beki Juuko Murshid na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji Laudit Mavugo

Mabadiliko yalionekana kuinufaisha Simba, ambapo walifanikiwa kupata bao la kusawazisha kunako dakika ya 66, kwa mpira wa kona kumfikia Laudit Mavugo akifunga kwa mguu na kufanya hadi dakika 90, zinakamilika Lipuli FC 1-1 Simba sc

Matokeo hayo yanaipa Simba sc, alama moja na kufikisha alama 59, ikiendelea kuongoza kwenye jedwali la ligi hiyo

Sambaza....