Tanzania ni moja ya nchi barani Afrika ambayo soka lake linakua kwa kasi sana, ndani ya miaka mitano ya hivi karibuni imekuwa na uwakilishi mzuri katika mashindano ya Kimataifa husasani katika ngazi ya vilabu yale yanayoandaliwa na shirikisho la mpira wa miguu barani afrika CAF yaani Ligi ya Mabingwa na Shirikisho.
Ligi ya Tanzania iko nafasi ya sita katika ligi bora Afrika ikiwa na point 56 nyuma ya Morrocco, Misri, Afrika kusini, Tunisia na Algeria na iko mbele ya Congo DR, Zambia na nchi nyingine za Afrika.
Ligi ya Tanzania ipo katika ile orodha ya mataifa kumi na mbili ambayo yanatoa wawakilishi wanne yaani wawili klabu Bingwa Afrika na wawili Shirikisho Afrika. Licha ya yote hayo lakini bado ligi yetu inakumbwa na ubovu na uchache wa viwanja bora.
Tanzania ina viwanja vitatu ambavyo vinamudu kuchezewa katika hali zote jua na mvua ( Benjamin Mkapa Stadium, uwanja wa Uhuru na Chamazi complex) angalau hivyo vinaweza kutumika katika michezo mikubwa ya Kimataifa, viwanja vingine vyote vilivobaki nchini vinaruhusu kuchezewa katika hali ya jua pekee.
Ubovu na ukosefu wa taa na uchakavu wa miundombinu ya uwanja wa Taifa na ule wa Uhuru unasababishwa na matumizi yaliyozidi kiwango kwani havitumiki kwa shughuli za soka pekee bali mpaka shughuli za kijamii kama vile semina, makongamano na mikutano jambo linalopelekea kuzidi kuchakaa kiasi kwamba viwanja hivi viko bize kutumika mda wote na hakuna ukarabati unaofanyika na hata ukarabati ukifanyika mara kwa mara na kila baada ya matumizi.
Viwanja vya mikoani hali ni tete ukarabati haufanyiki kwa wakati, kiasi baadhi ya vingine kukosa sifa za kimashindano hadi kufungiwa mfano Mabatini pale Pwani, Jamhuri pale Dodoma, Mkwakwani pale Tanga n.k.
Serikali kupitia Chama cha Mapinduzi hushikilia viwanja karibia vyote vya mikoani basi hawana budi kuvifanyia ukarabati wakati huu ligi inakwenda mwishoni ili ligi itakapoanza mwezi Agosti viwanja viendane na hadhi za kimashindano kwa mfano wanaweza kuingia ubia na baadhi ya makampuni ili kuboresha viwanja, mfano kwa kuwapa haki za umiliki au kuuza haki za majina ya viwanja.
TFF na maafisa wake wafanye matembezi na ukaguzi wa mara kwa mara viwanjani kuepuka ukiukwaji wa kimaagizo ya marekebisho wanapoyatoa kwa wamiliki wa viwanja.
NB :ligi bora bila viwanja bora ni kuunajisi mpira.