Sambaza....

Ulee uhondo uliokosekana kwa muda mrefu kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya corona sasa wakati wowote unarudi baada ya Mh. Rais kusema anafikiria hata kuirudisha ligi ichezwe kama kawaida ili watu wakae nyumbani kwao kuangalia mpira bila kwenda uwanjani.

Tayari Bodi ya Ligi imeshaanza kuweka mikakati ya kurudisha ligi huku kipaumbele ikiwa ni kucheza michezo hiyo bila ya watazamaji, kwa maana michezo itaonyeshwa kwenye TV pekee.

Mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Azam fc na Lipuli fc.

Lakini pia Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Harisson Mwakyembe tayari ameiagiza TFF kuweza kuwasiliana na FIFA ili kuona kama wataweza kupata msaada wowote pindi ambapo wanafikiria kumalizia ligi. Na kwa upande wao pia kama wizara husika nawao watakua na mipango madhubuti kuhakilisha ligi inachezwa na

Ikumbukwe baada ya Ligi kusimama kutokana na ugonjwa wa corona baadhi ya wachezaji wa kigeni wanaozitumikia klabu mbalimbali hapa nchini waliondoka na kwenda makwao hivyo kama ligi ikirudi tena huenda baadhi ya timu zikaathirika na kuwakosa wachezaji wao muhimu.

Mlinda mlango wa KMC ambae ni raia wa Burubdi Jonathan Nahimana.

Vilabu kama KMC, Azamfc, Simba na Yanga watawakosa wachezaji na makocha wao kutokana na nchi nyingi kufungwa kwa viwanja vya ndege na hivyo kufanya kuwa na wakati mgumu kupata usafiri wa kurudi nchini.

Baadhi ya klabu tayari zimeanza kufanya taratibu za kuwarudisha wachezaji wao haswa wanaotoka nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Uganda na Zimbabwe hata kwa njia ya basi ili waweze kurejea na kumalizia Ligi Kuu Bara. Hata hivyo pindi watakaporejea watatakiwa kukaa siku 14 karantini kabla ya kuruhusiwa kujiunga na wenzao moja kwa moja.

Haruna Niyonzima akimiliki mpira mbele ya Clatous Chama

Baadhi ya wachezaji na watu wa benci la ufundi wanaotarajiwa kukosekana ni pamoja na Meddie Kagere, Clatous Chama, Francis Kahata (Simba sc),  Razack Abarola, Yakub Mohamed, Daniel Amoah, Aristica Cioaba (Azam fc), Luc Aiymael (Yanga sc).

Sambaza....