Sambaza....

Jana Yanga imepata sare katika mchezo wa mkondo wa kwanza katika hatua ya kwanza ligi ya mabingwa barani Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, Zahera amewapongeza wachezaji wake kwa mchezo mzuri.

“Kwa ujumla timu imecheza vizuri, wachezaji walijaribu kutumia nafasi tulizotengeneza”

“Matokeo haya hayatukatishi tamaa kwani bado nafasi ya kufanya vizuri ugenini tunayo”

“Tunapaswa kufunga bao nchini Zambia, hata kama tungeshinda bao 1-0, bado tungepaswa kufunga bao ugenini, tutakwenda kuwafunga huko huko kwao,” amesema Zahera

Matokeo ya leo hayana tofauti na matokeo ya mchezo wa hatua ya awali kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa ukiisha kwa sare ya bao 1-1

Hata hivyo Yanga ilifanikiwa kushinda kwa bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa nchini Botswana

Bado Yanga imeendelea na mwenendo wake wa kutofanya vizuri kwenye michezo ya nyumbani lakini kupata matokeo inapocheza ugenini.

Zahera amzungumzia Kamusoko

Kiungo wa zamani wa Yanga Thabani Kamusoko ndiye aliyefunga bao la kusawazisha la ZESCO kwenye dakika za majeruhi

Zahera amesema kiungo huyo alitumia vyema nafasi aliyopata, hata hivyo hakuipa usumbufu wowote timu yake.

“Kamusoko ni mchezaji wa kawaida sana, hakutusumbua kabisa ila yule namba 25 na Winston Kalengo walikuwa mwiba kwetu,”

Baada ya mchezo huo kumalizika, timu hizo mbili zinatarajiwa kurudiana Ndola nchini Zambia tarehe 27, siku ya Ijumaa ya mwezi huu kakamilisha hatua hii.

Sambaza....