-Ligi Kuu Bara inafikia tamati leo May 27 huku mbivu na mbichi zikijulikana kabla ya saa 12 jioni. Nani kushuka nani kubaki na nani kucheza Playoffs.
-Tayari African Lyon imeshashuka daraja na Simba sc wametwaa ubingwa kwa alama zao 92 mpaka sasa.
-Yanga, Azam fc, KMC, Mtibwa Sugar, Lipuli fc, Ndanda, Allince fc, Mbeya city na Coastal Union zina uhakika wa kushiriki TPL msimu ujao.
-Mwadui, Kagera Sugar, Tanzania Prisons, Ruvu Shooting na JKT Tanzania lazima washinde michezo yao ya leo ili kujiweka angalau katika nafasi ya kucheza Playoffs au kusalia Ligi Kuu Bara
-Singida utd, Biashara united na Mbao fc pia hawapo salama na wanahitaji ushindi wa hali na mali ili kusalia msimu ujao.
-Michezo yote itacheza muda mmoja yani saa 10 kamili jioni isipokua mchezo wa Simba pekee utachezwa saa tisa kamili.
Kati ya timu sita zilizopanda mwaka jana ni timu za KMC, Coastal Union, Allince School ndio zipo salama huku Biashara, JKT Tanzania zikipambana kusalia Ligi Kuu Bara, African Lyon wao wameshashuka daraja tayari.
-Azam tv wenye haki ya kurusha matangazo wapo tayari kurusha mubashara michezo sita kati ya kumi inayochezwa leo.
-Michezo sita itaruka live huku mingine minne ikirekodiwa. Baadhi ya mechi zitaonyeshwa Azam HD, Azam one na two, Sinema zetu na Azam Extra.
Baadhi ya nyota wapya na chipukizi wameibuka katika timu mbalimbali na kugeuka msaada mkubwa kwa timu zao.
-Chipukizi kama Tariq Seif (Biashara utd), Salim Aiyee (Mwadui fc) Dick Ambundo (Allince Fc), Ramadhani Kapera (Kagera sugar), Ayoub Lyanga (Coastal Union) na Vitalis Mayanga (Ndanda fc).
-Huku baadhi yao wakitegemewa kuziokoa timu zao haswa katika michezo hii yamwisho. Nyota kama Tariq, Aiyee na Kapera wakitarajiwa kuzibeba Biashara, Mwadui na Kagera.
-Mchezo wa Mtibwa na Simba ndio ambao utatumika kumkabidhi Simba kombe lake la ushindi la Ligi Kuu Bara.
-Mpaka sasa haijulikani bingwa wa msimu huu (Simba Sports Club) watakabidhiwa zawadi gani na Bodi ya Ligi.