Sambaza....

Mchezaji wa zamani wa Liverpool John Barnes amependekeza kuwa Kylian Mbappe sio usajili sahihi ambao kocha wa Liverpool  Jurgen Klopp angetakiwa kuufanya katika majira ya kianganzi wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa. Barnes anaamini Klopp anapaswa kuangalia machaguo mengine na si kwa nyota huyo wa Ufaransa.

John Barnes ambae ni mzaliwa wa Jamaica ametoa maoni yake na kusema “Watahitaji kusaini mchezaji mwingine eneo la ushambuliaji wakati fulani ikiwa moja ya wachezaji  watatu wa mbele wataondoka. Kylian Mbappe ni mzuri kwenye mpira lakini angefanya mambo mengine(akiwa hana mpira)? Nadhani kama wewe ni nyota wa miaka 21, mtazamo wako hautabadilika.”

Kylian Mbappe

Barnes ambae alikua akicheza kiungo wa pembeni wakati wa enzi zake ameongeza: “Asilimia tisini na tisa ya watu hawangewachagua (Jordan) Henderson na (Georgiainio) Wijnaldum mbele ya Kevin De Bruyne na David Silva au hata Jack Grealish au James Maddison, lakini (Wijnaldum, Henderson) wanaifanyia kazi Liverpool.  Divock Origi na Xherdan Shaqiri waliingia katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Barcelona, ​​uwezo  wao ulikuwa mzuri na walikuwa tayari kwa mwili. Inaonyesha walikuwa wakifanya mazoezi vizuri, wakingojea nafasi yao.”

John Barnes aliitumikia Liverpool kwa miaka 10 kuanzia mwaka 1987 mpaka mwaka 1997 , huku pia akiwa amepitia vilabu vingine Uingereza kama Watford, Newcastle na Charton Athletics.

 

Sambaza....