Mwaka2005 vijana-wapenda soka mtaa wa Area Six-NaneNane, Morogoro tuliamua kuiingiza katika ligi rasmi timu ya mtaani kwetu.
Kulikuwa na vijana zaidi ya 35 wenye vipaji vya soka. Na kati yao tulikuwa wawili tu waliokuwa tukicheza nje ya mtaani kwetu kila msimu wa ligi ya TFF ( ligi daraja la nne- daraja la pili).
Wazo la kuisajili timu lilikuja baada ya kumalizika kwa ligi ya mbuzi mnyama ambaye Pamoja na kuingiza timu mbili kutoka mtaani hapo- zote zilifanikiwa kufika nusu fainali, na New Kings niliyokuwa naichezea ilitwaa ubingwa.
– Sporting Club Lisbon ( Ureno)
– Benfica Sporting Club ( Ureno)
– Sporting Lokeren ( Ubelgiji)
– Al Ahly Sporting Club ( Misri)
– Asante Kotoko Sporting Club ( Ghana)
– Sports Club Villa ( Uganda)
Tukaitisha kikao, tukafikia mwafaka lazima tuisajili timu moja, na tukaafikia itabeba jina la mtaa tunaotokea. Tukaiita Area Six Sports Club.
Tukaingia mtaani kuchangisha nyumba hadi. Tukaenda MRFA. Kama nahodha wa timu, nilikuwa bega kwa bega na viongozi wawili tuliowachagua sisi kama wachezaji.
Naendelea kumshukuru sana Jimmy Lengwe ambaye hivi sasa ni katibu msaidizi wa Chama cha Soka Mkoa wa Morogoro. Wakati huo akiwa katibu mkuu wa cha cha soka manispaa ya Morogoro ( MDFA), Lengwe alitusaidia kuandaa katiba na kikubwa alitusisitiza kutotumia jina la Sports Club na kutumia Football Club.
Nilimuuliza kwanini? Akaniambia Fifa wanahitaji klabu za mpira wa miguu tu na si michezo mingine. “Sports Club inamaanisha klabu yenu itakuwa ni mikusanyiko ya michezo mingi si soka pekee na Fifa wapo kwa ajili ya mpira wa miguu pekee.” nakumbuka sehemu ya majibu ya Lengwe.
” Hata hizo Yanga na Simba zitakuja kubadilika majina ya mwisho na watalazimika kutumia Football Club. ”
– FC Barcelona ( Hispania)
Klabu hii ya ulaya pia ina timu za michezo mingine kama Basketball, Volleyball na n.k. Umaarufu huu wa Barcelona unatokana na mafanikio makubwa ya timu yao ya soka.
Je, Young Africans Football Club itazuiwa kuwa na timu za Netball, Masumbwi na michezo mingine?
#Itaendelea