Idadi ya wachezaji wa kigeni wanaoweza kusajiliwa na timu moja mpaka sasa ni 10, lakini wapo wanaoamini ni idadi kubwa sana huku wakitaka ipunguzwe wakiwa na sababu zao na pia wapo wanaoona ni sawa kuwa na idadi hiyo kubwa kwa timu moja.
Pande zote mbili wana hoja na sababu zao katika kutoa utetezi wa idadi hiyo ya wachezaji na afya ya soka letu. Na kwa pande zote hizo sababu zao zina maana na zina msingi kabisa kwa ustawi wa soka letu na timu ya Taifa.
Kwa misimu miwili hii kwa maana ya msimu uliopita 2018/2019 na msimu huu 2019/2020 ambao haujafika tamati bado kuna toafuti katika swala la ufungaji wa mabao kwa wachezaji wakigeni na wazawa.
Ukitazama misimu yote hiyo unaona kwanza kabisa mfungaji bora ni raia wa kigeni(msimu uliopita) (Meddie Kagere- Simba sc.) Lakini pia mpaka sasa ndie kinara akiwa na mabao 19.
Katika chat hapa chini utaona ni jinsi gani vinara wa ufungaji ni wachezaji wa kigeni kwa maana ndio wenye mabao mengi kushinda wazawa.
Lakini pia kwa kinachoonekana hapo katika misimu hii miwili ni kukosekana kwa muendelezo mzuri wa wachezaji wazawa “Consistency”. Ni wachezaji wawili au watatu tu ambao mpaka sasa angalau wameweza kufanya vizuri misimu yote miwili. Wachezaji hao ni Ayoub Lyanga (Coastal Union) Idd Nado (Azam fc) Fully Zullu Maganga (Ruvu Shhoting).
Kwa upande wa pili unaona mchezaji kama Salim Aiyee katika msimu wa 2018/2019 alifunga mabao 18 lakini kwa msimu huu ana bao tu mpaka ligi inasimama. John Bocco alimaliza msimu uliopita na mabao 16 lakini kwasasa ana mabao manne tu.
Ukitazama kwa wachezaji wakigeni utaona kuna wachezaji Meddie Kagere na Bigirimana Bleise ambao msimu uliopita walifanya vizuri na pia msimu huu pia bado wanafanya vizuri. Katika kundi hilo la wageni yupo Obrey Chirwa pia ambae msimu uliopita 2018/2019 (magoli3) ulikua mbaya kwake lakini msimu huu (ana mabao 8 mpaka sasa) ametokea kufanya vizuri. Katika kundi kuna Donald Ngoma ambae amekua na msimu huu mbovu akiwa na mabao mawili tu mpaka sasa.
Huku namba wachezaji wa kigeni waliofanya vizuri katika ufungaji wa mabao wakiwa wameondoka nchini kina Emmanuel Okwi na Heritier Makambo.