Jana kulikuwa na mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara katika uwanja wa Sokoine kati ya Mbeya City na Yanga.
Katika mchezo huo ulimalizika kwa timu zote kutoka sare ya goli 1-1, kuna mengi yaliyotokea ikiwemo vurugu ambazo zilianzishwa kwenye mchezo huo.
Lakini kuna tukio moja ambalo lilitokea katika mchezo huo ulipokuwa unaelekea mwishoni.
Kabla Mbeya City walikuwa tisa (9) kwani dakika ya 70 mchezaji Bakari Malima wa Mbeya City alipewa kadi nyekundu.
Na katika dakika ya 96 mwamuzi wa akiba alionesha kibao cha mabadiliko, Eliud Ambokile jezi namba kumi (10) alitakiwa apumzike na mchezaji mwenye jezi namba kumi na sita (16) alitakiwa aingie.
Wakati mwamuzi wa akiba akionesha kibao cha mabadiliko Eliud Ambokile alikuwa anapatiwa huduma ya kwanza nje ya uwanja alipata majeraha kidogo. Baada ya kumaliza kupatiwa huduma ya kwanza aliomba kuingia na mwamuzi wa kati akamruhusu kuingia.
Na kufanya idadi ya wachezaji wa Mbeya City ndani ya uwanja kuwa kumi(10) badala ya tisa (9).
Hivo Mbeya City walinufaika na mabadiliko hayo kwa takribani dakika moja. Yanga kwenye hili wana haki ya kulalamika na wanahaki ya ya kusikilizwa na kupewa haki yao stahiki.
Kutojua sheria sio utetezi kwenye kesi yoyote ile, kosa limetokea hakuna bahati mbaya kwenye kosa na hii inanikumbusha tukio ambalo liliwahi kutokea hapa hapa Tanzania msimu wa 2014/2015
*Kagera sugar vs Rhino rangers* mchezaji wa Rhino alipewa kadi nyekundu hivyo Rhino waliimuingiza mchezaji mwingine, katika mazingira ambayo aliyetokewa hakujua hivyo wakaendelea kucheza wakiwa na wachezaji kamili 11 uwanjani.
Mechi ikiisha kwa sare ya 0-0. Baada ya Mechi TFF waliamua kuipa Kagera goli tatu na point tatu kwa kosa lifuatalo.
Rhino wamevunja sheria kwa kuchezesha wachezaji 12 katika kwa wakati Mmoja uwanjani bila kufanya mbadiliko na ni kinyume cha sheria na kanuni za soka.
Hivo kwenye tukio la mechi ya jana Yanga wanahaki ya kulalamika , kusikilizwa na kupewa alama zao tatu.