Mpira wa miguu ndio mchezo pendwa zaidi ulimwenguni, ni mchezo ambao haubagui wafuasi yaani wazee, vijana na hata watoto wanauishi mchezo huu.
Lakini mchezo wa mpira wa miguu inasadikiwa kuwa moja ya michezo hatari zaidi ulimwenguni kwani hatari na ajali nyingi hutokea pindi uchezwapo, baadhi ya wachezaji hupoteza maisha na wengine hupata majeraha na ulemavu wa kudumu.
Usalama wa wachezaji ni suala la msingi sana, kwamfano katika nchi zilizoendelea sana kisoka husuani nchi za Ulaya usalama wa mchezo na wachezaji umekua ukipewa kipaumbele kikubwa kiasi kwamba hatua za msingi zimechukuliwa mfano ukatajwi BIMA kwa wachezaji, hii ililenga kumlinda mchezaji dhidi ya ajali zote akiwa kazini (mchezoni) na hata nje ya mchezo.
Baadhi ya mashirika na mabenki yameingia ubia na ligi kudhamini BIMA za wachezaji.
Stori ni tofauti hapa kwetu, ligi yetu inasifika na ni moja ya ligi bora kubwa kumi barani Afrika, lakini suala la usalama wa wachezaji ni mdogo sana, wachezaji hawana BIMA za afya.
Wachezaji wapatao ajali wawapo mchezoni hugharamiwa na vilabu vyao na wengine hujiuguza wenyewe kwa gharama zao, hii imekua kikwazo kwa maendeleo ya wachezaji wetu hususani wazawa. Sio shirikisho wala vilabu nchini ambavyo huwakatia BIMA wachezaji wao ili kumudu gharama za matitabu endapo watafikwa na ajali mchezoni.
Muamko ni mdogo sana ni kama bado tuko usingizini juu ya hili mfano wapo wachezaji nchini wamepata ajali lakini kwa sababu ya kutokuwepo kwa BIMA wamekuwa wakitangatanga na kuomba msaada wa matibabu huku na kule, mfano Gerald Matias Mdamu mchezaji wa polisi Tanzania alipata ajali ya gari akiwa na timu wakielekea mazoezini, kama angekuwa na BIMA ya uhakika basi angetibiwa kwa wakati pengine angerudi uwanjani.
Nini kifanyike?
▪ Elimu itolewe kwa vilabu na wachezaji juu ya umuhimu wa BIMA za afya; Hapa vyombo vya habari na waandishi wa habari waisogeze agenda hii juu ya umuhimu wa BIMA za afya, lakini pia shirikisho pamoja na washika dau washikane kuhakikisha vilabu pamoja na wachezaji wanakata bima za usalama wa afya.
▪Shirikisho la soka lichukue hatua za makusudi kuhakikisha upatikanaji wa Bima kwa wachezaji. Kwamfano shirikisho la soka la Cameroon linaloongozwa na Gwiji Saumuel Etoo, limeingia makubaliano na mabenki pamoja na mashirika kuhakikisha wachezaji wote wanaocheza ligi nchini Cameroon wanapatiwa Bima za afya hususani wazawa.
Hivyo hata TFF wanaweza kama wataamua sasa kwa kuingia katika makubaliano na baadhi ya mabenki na washirika banafsi ili kudhamini Bima za afya kwa wachezaji.
▪Vilabu pia vichukue hatua stahiki ili kuhakikisha wafanyakazi na wachezaji wanapatiwa Bima za afya, hii itasaidia kuwaokoa na gharama za matibabu pindi wapatapo ajali.
NB: Inawezekana tumechoka maharage lakini kama tunataka nyama tusubirini kwanza banda lijae.