Wapwa hili ndio andiko langu lakiufundi la mwisho kutoka katika kile nilichokiona katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika siku ya Wananchi katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir.
Hawa Nchimbi na Kaseke ni wapiganaji watu wanaozaliwa kwenye mlengo wa” born to win” ni wapambanaji mno kwa timu yao (Wazee wa Fluku) ambazo timu wakititumia watanufaika nao sana.
Kaseke moja ya viungo wachache wa pembeni ambao ni tipicle wakabaji anachangia sana kwenye balance ya timu hasa timu inapopoteza mpira kwa aina za uchezaji wao ukiwajaji kwa magoli hautakuwa sahihi hapa unapaswa kuwatizama kwenye “ability of doing work”.
Nategemea hichi ndio kikosi kilicho anza tukipata nafasi tutagusa walioingia kipindi cha pili na tulichokiona kwao.
Hitimisho langu Yanga ina squad yenye vipaji vikubwa ni jukumu la moja kwa moja la benchi la ufundi kuweza kunganisha vipaji vyao na pia kuimplement mbinu zitakazowapa point tatu kiwepesi ili kuweza kufanya vizuri ikiwemo suala la umoja ndani ya timu na treatment zisizo na matabaka wanaweza kufanya jambo
Vikorombwezo vingine ndani ya game ya Jana ni akina Fei wawili” Fei na Fei” sijui kama umlimtizama kiungo jezi no 6 wa Aigle Noir Yanick Nkurunzinza jamaa ni fundi anacheza kwenye the same type ya Fei japo yeye anapewa support na kiungo mwingine jezi no 13 Merse Masoud kwa combination yao hao Warundi wawili ilinikumbusha ya Xavi na Iniesta.
Pia hili mdogo wangu Ditram Nchimbi atanijibu kwanini amebadilisha jezi yake toka aliyojibrand nayo no 29 akavaa 2 then Tuisila akavaa 29 ,ni ridhaa yake au imeamriwa hivyo kivyovyote vile nitapaswa kujua maana yake.