Sambaza....

“Tp Mazembe imekamilisha usajili wa Eliud Ambokile kutoka Mbeya city”,asubuhi moja niliona kichwa cha habari cha gazeti fulani kuhusu masuala ya usajili nikajua ni zile zile habari za kuuza magazeti, siku kadhaa mbele niliona gazeti kwa rafiki yangu lililoandikwa “Ramadhani Singano atua TP Mazembe “ niliamua kufuatilia sasa zile habari na niliposoma niligundua ni kweli sajili hizo zimefanyika.

Ghalfa nikakumbuka sakati la Ibrahimu Ajib na Mazembe hapo nikagundua hili ni anguko jipya la Mazembe sasa rasmi utawala wao katika ukanda huu utaanza kupotea.

Kwanini niliamini hivo sio kwa sababu wamemsajili Singano au Eliud lakini je sajili hizo zina tija kwao? Mazembe walimsajili Singano akiwa kaachwa na Azam kwa madai ya kushuka kiwango lakini pia Ambokile huyu ambae anacheza Mbeya city ya kawaida sana na hata kama wana uwezo mzuri lakini sio wa kwenda kucheza TP Mazembe wanafainali wa Klabu bingwa ya Dunia dhidi ya Inter milan ya Etoo.

Ndio ulikua muda wa anguko na kweli zile sajili hata hazikucheza Singano akatolewa kwa mkopo Ambokile akarudi zake Mbeya City na mpaka leo hadithi zao ziliishia hapo.

Eliud Ambokile

Mukoko aliwahi kuwa tegemezi pale Yanga, lakini ilikua Yanga ya Yikpe, Nchimbi na wenzao kadhaa ambao walikua ni wachezaji wa kawaida waliochezea timu kubwa, Yanga walipoanza kufanya mabadikiko Mukoko alikua moja ya wachezaji iliyowaacha kwa madai ya kutokubaliana maslahi, lakini naamini kama Yanga wangemhitaji basi wangempa anachotaka.

Hii inaonesha waliona anachohitaji na anachoipa timu haviko sawa wakaachana nae, lakini leo Mukoko ni moja ya wachezaji tegemo pale Mazembe timu ambayo ina anguko kubwa la kiuchumi na kiuchezaji hii si Mazembe ambayo ingeweza kumfunga Simba bao tatu kwa mbili pale kwa Mkapa huku Samata akiibuka kidedea kwa kufunga goli la mwaka lililompa mkataba kwa Katumbi.

Mukoko Tonombe.

Mazembe bado wanajitafuta sitashangaa Yanga akipata sare pale Lubumbashi, ushindi wa Yanga kwa Mazembe ni ishara ya kuanza safari ya mafanikio kwa uzuri lakini pia ni kengele ya tahadhari kwao kutobweteka na ushindi dhidi ya timu inayojitafuta.

Tembo hata akonde vipi hawezi kuwa mbu, lakini ilikuwa mechi ya Mazembe yenye anguko dhidi ya Yanga yenye muamko, wachezaji wazuri ndio chachu ya mafanikio katika klabu lakini Mazembe kwa sasa ina wachezaji wazuri wasiozidi watano ambao wanaweza kucheza katika klabu zetu hapa Tanzania.

Mashabiki wa Yanga wakishangilia Benjamin Mkapa Stadium.

Vita ya Real Bamako ni vita ngumu kwa Yanga kwa timu hii yenye alama moja kwenye kundi huku akimsubiri Yanga nyumbani. Yanga ana mechi ngumu dhidi ya Mazembe pale Lubumbashi halafu akimaliza dhidi ya Monastir pale Lupaso anatakiwa kuchanga karata zake vyema sana katika mechi nne zilizobaki.

Kimahesabu, hesabu zinambeba Yanga lakini dakika tisini ndo huamua mchezo.

Kila lakheri Yanga kil lakheri Wananchi!!

Sambaza....