Sambaza....

Jana rasmi Al-Ahly wamekata tiketi yakucheza fainali ya klabu bingwa Afrika, wakifanya hivyo mara ya tatu mfululizo chini ya kocha Pitso Mosimane.

Wydad pia anarudi tena katika utawala wa Afrika kwa kutinga fainali baada ya kumfunga Petro Luanda kwa ushindi wa jumla na kutangulia fainali itakayopigwa nchini kwao Morroco.

Mshambuliaji wa Wydad Casablanca akimtoka mlinzi wa Petro Luanda.

Tazama jinsi wababe hao walivyotinga fainali, wote wawili wamepata matokeo katika viwanja vya ugenini, Al Ahly alitoa sare nchini Algeria ya mabao mawili kwa mawili wakati Wydad wao walishinda kabisa tena bao tatu ugenini Angola.

Al-Ahly katika mchezo wa ugenini dhidi ya Es Setif walilazimisha sare ya mabao mawili kwa mawili baada ya mchezo wa kwanza kushinda nne bila, wakati Wydad Casablanca wao walishinda mabao matatu kwa moja dhidi ya Petro Luanda kabla ya kumaliza kazi nyumbani kwa sare ya bao moja kwa moja nyumbani.

Kiungo wa Al Ahly akipiga shuti mbele ya walinzi wa ES Setif

Simba licha ya kutolewa katika robo fainali ya klabu bingwa Afrika mara mbili na Shirikisho mara moja lakini bado hakupoteza nyumbani alikwenda kufia hukohuko ugenini.

Simba wamekua wakitumia vyema uwanja wao wake wa nyumbani kitu ambacho vilabu vingi vya Afrika vimeonyesha kushindwa haswa hao waliotinga nusu fainali ya klabu bingwa Afrika.

Akiwa kwa Mkapa ameangusha vigogo wakubwa wa Afrika ambal wanafanya vyema katika michuano hii mikubwa Afrika.
Ni TP Mazembe pekee ndio wakifanikiwa kuibishia Simba na kutoka salama kwa Mkapa baada ya kupata suluhu.

Zana Coulibaly akimdhibiti mlinzi mshambuliaji wa TP Mazembe.

Lakini vigogo wote Afrika Al-Ahly, AS Vita, RS Berkane, Asec Mimosa na Al Hilal walivuta pumzi ya moto Benjamin Mkapa.

Hata Orlando Pirates na Kaizer Chiefs waliofanikiwa kuiondoa Simba katika robo fainali wote walipata tabu kwa Mkapa baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Simba.

Benard Morrison akimuacha chini mlinzi wa Kaizer Chiefs.

Simba ni miongoni mwa timu za Afrika zinazojua kutumia kiwanja chake cha nyumbani vyema kabisa katika michuano hii ya Afrika.

Natamani Simba wakutane na vigogo wengine kama Mamelody Sundowns, Esperance na Wydad Casablanca nione kama wataendeleza ubabe wao kwa Mkapa kwa ma-giants wa Afrika.

Sambaza....