Unamkumbuka Marcio Maximo? Kocha wa zamani wa Taifa Stars na baadae Yanga Sc.. Pitia moja ya makala hii ambayo iliandikwa kipindi hicho na Dizo Moja (2009).
Asalaam Aleikum ewe mtanzania mwenzangu ambae umekata tamaa na hali ngumu hii ya maisha magumu kwa kila mtanzania aishiye maisha ya tia mchuzi pangu pakavu –sehemu kuu ambayo huwa anajifariji Mtanzania huyu ni kwenye mpira wa miguu maarufu kama Soka. Watanzania wanasahau juu ya maisha magumu pale tu habari za Soka zinapoongelewa wanasahau juu ya mikata mibovu inayoididimiza nchi kwa sasa pale tu Soka inapochukua nafasi yake.Soka imekua kama ibada na sio kwa Tanzania pekee bali ni Dunia nzima kiasi hata Wamarekani ambao kwao Soka ulikuwa ni mchezo wa nne au tano kwa kupendwa sasa umekua ukikua na kupendwa.
Twende kwenye mada yetu hapo juu isemayo Marcio Maximo wewe ni bonge la kocha lakini…… Mengi yamesemwa juu ya uwezo wa ufundishaji wa Mbrazili huyu wengine wakidai uwezo wake umeishia pale, wengine wakidai hana jipya na wapo ambao bado wana imani nae kuwa bado anaweza kutuwezesha kutamba wakiwemo viongozi wa ngazi za juu wa TFF ila katika hili siwezi kuwa na uhakika na yale wanayosema yana ukweli au ni aina ya kumkingia kifua huku mioyoni wanaumia.
Nikionacho mimi juu ya Kocha huyu ni Kocha bora sana ila ni binadamu wa kawaida kama binadamu wengine wakawaida walivyo. Maximo anakosea ndio anakosea yeye ni binadamu na kukosea ni sehemuya maisha ya binadamu hivyo akikosea kukosolewa ni lazima na pindi anapokosolewa viongozi wa TFF msione ni kumkosea heshima Kocha bali yeye hawezi kuwa na vitu vyote jamani Maximo sio Mungu yeye ni binadamu kama wengine. Maximo kwa ili unakosea kumchukua AliMustapha “Bartez” na kuwa Golikipa wako namba moja kwenye mechi dhidi ya Misri ni uvunjifu wa heshima kwa makipa wengine wanaocheza kila mechi kwenye timu zao kila wiki na kupata matokeo bora hata kama sio bora. Maximo kwa lile ulitokota kumchezesha Erasto Nyoniikiwa mechi pekee aliyocheza ni dhidi ya Simba SC tena akiingia kipindi cha pili dakika za mwisho. Kumchezesha Mwinyi kazimoto akiwa ndio kwanza ametoka majeruhi ni kumuua mchezaji kisaikolojia pindi akifanya vibaya litakua jinamizi limfuatalo kipindi chote cha uchezaji wake wa soka.
Uteuzi wa wachezaji wa mbrazili huyu nao ni tatizo, hatukuelezwa sababu zilizomfanya amuache Golikipa Shaaban Kado kwenye msafara wake wa Misri na Yemen. Sijui kwanini unamuita Shedrack Nsajigwa kwenye Kikosichako ikiwa ameonyesha kila dalili ya kuchoka .
Maximo acha kutembelea nyota yako wachezaji waliokupa mafanikio wamechoka hivyo inabidi ubadilike Baba. Kila siku unasema una kundi kubwa la wachezaji kwenye mafaili yako watanzania wanakaribia kukuchoka shtuka mapema angalia alama za nyakati. Kila siku unahubiri “ U-profeshno” ambao kwa mtazamo wangu wewe unaukosa huo ‘’U-profeshno’’ Maximo profeshno yoyote yule hawezi kuwa na Chuki, Gubu, Visasi, Asiye shaurika na mambo mengine mengi ambayo unayo nadhani ungeachakuhubiri habari hizo za ‘’uprofeshno’’ .
Kocha Mkuu wa Kongo maarufu kama Obama alishatoa maoni juu ya kikosi chako baada ya kukupiga bao mbili bila majibu pale uwanja mpya wa Taifa sidhani kama uliufanyia kazi au ndio niamini haushauriki kama vyombo vingi vya habari vilivyopata kuripoti kipindi cha awali.
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ghana Ratomir Rajevackwa imani yake kubwa aliyokuwanayo kwa kiungo na nahodha wa timu hiyo Stephen Appiah alikua akimjumuisha kwenye kikosi chake cha timu ya Taifa mara zote alipoita timu lakini alikua hampangi kucheza mechi yoyote kutokana na kufahamu kuwa Appiah hana timu anayochezea hivyo uwezo wake wa uchezaji hautakuwa bora kutokana na kukoasa mechi za ushindani japo alikua nae mazoezini mara zote a;ipomuita lakini hakumchezesha na ili kumlinda mchezaji wake hakumtwisha mzigo mzito kwenye mechi yoyote kwasababu kufanya vibaya kwa mchezaji uliyempa majukumu mazito ni kumuua kisoka.
Maximo umetuletea Mohamed Mwarami “ Shilton” kwa maoni yangu Maximo hilo nalo umechemsha vibaya kutokana na sera yako ya kukuza vijana “Shilton” hawezi kufaa kwenye mipango yako tayari ni mzee sana usipoteze muda na pesa ya Taifa kumleta mchezaji ambae hatofaa kwa mipango yako. Nakumbuka ulienda Sweden na Denmark na kumleta Michael Chuma ambae hakudumu kwenye timu yako ilhali anacheza soka hukohuko lakini ulipomleta wadadisi wa mambo tulijua hawezi kufaa na ikawa kweli. “Shilton” ni mzee na kwa saa anamalizia soka tu huko Msumbiji na bado hana ubora wa kumfanya awe golikipa namba moja wa starz. Vipi kuhusu bwanamdogo Razack Khalfan yule bwana mdogo mwenye kipaji cha hali ya juu kutomjumuisha kwako? Sera nyingi za makocha wengi ni kutozungumzia wachezaji ambao hawajawachagua kwa timu ya Taifa japo wanaonekana bora kwa timu zao,hili nalo ni tatizo kwako Marcio Maximo.
Mechi ya Misri ulitaka wachezaji wacheze huru labda lakini je aina ya wachezaji uliokua nao siku ile na aina ya timu uliyokua unacheza nayo vilishabihiana? Jibu hapana,
Misri walifanya kila kitu , wakatufunga kwa krosi , kwa faulo na kutuonyesha kuwa bado tuna safari ndefu na Mlima mrefu sana wa kuupanda kuelekea huko kwenye mafanikio.
Maximo jua kwa sasa watanzania wanaufahamu mkubwa wa mambo ya Soka na sio ubabaishaji. Watanzania wanataka kuona timu inafungwa kimpira na sio kwa makosa ya kizembe tena mtu ya mtu mmoja au wawili waigharimu timu. Kwa waliofuatilia matangazo yaliyokua yanarushwa na TBC1 kutoka katika mji wa Aswan japo hayakuwa ya moja kwa moja na wakiwa tayari washajua matokeo ya mechi ile baada ya kituo kimoja cha redio kutoa habari za matokeo yale walishuhudia nini kilichijiri na wakati Misri wanafunga bao la nne alionekana KelvinYondani kurusha mikono juu hewani kwa hasira baada ya kuona wamefanya kazi ngumu lakini wanafungwa kirahisi huku wakiamini kuwa hawastahili kufungwa magoli hayo.
Maximo wewe ni bonge la kocha nakila nchi ingependa kuwa na wewe kwa sababu Umesaidia kuinua ari ya mapenzi kwa timu ya Taifa ambayo ilishapotea, Umesaidia kuhamasisha mauzo ya jezi za timu yetu ya taifa na watanzania kwa sasa wanavaa Jezi hizo pindi timu yetu inapocheza nje ya nchi au ndani ya nchi, Umesaidia kufanya timu yetu ya taifa icheze soka linaloeleweka,Umesaidia kutufanya siasa za FIFA kutuweka juu kwenye viwango vya ubora duniani japo kihalisi tupo nyuma sana.Umefanya mengi ikiwamo wachezaji kuheshimukambi ya starz tofauti na miaka ya nyuma na mambo mengine mengine.
Maximo wewe ni bonge la kocha lakini jua siku hazigandi watanzania wamechoka kungoja na kwa bahati ya pekee katika historia ya nchi hii inawezekana wewe ndie kocha wa pekee kukaa muda mrefu kwenye kiti hicho na pia ndio kocha wa pekee ambaye maamuzi yako hayaingiliwi na viongozi wa soka na serikali ni kocha ambaye amefanya kazi katika kipindi cha Neema kuliko wengine wote waliopita toka nchi hii ipate uhuru.
Maximo ni wewe tu ambae unaweza kusema timu iingie kambini au la ni wewe tu ambae umeshapangua ratiba za ligi kuu mara kwa mara ili upate nafasi ya kukaa kambini na timu kwa muda mrefu kuliko kawaida ya timu nyingine nyingi za taifa .
Maximo ni wewe tu unaeweza kusema timu ishiriki mashindano Fulani au isishiriki kama tulivyoona TFF ikikataa kupeleka timu ya Taifa Zimbabwe kwenye mashindano ya Cosafa- Castle ikiwa ni mualiko toka shirikisho la mpira wa miguu la kusini mwa Afrika COSAFA.
Maximo una mengi ya kuamua lakini umefika muda sasa unatakiwa ufanye maamuzi yenye tija kwa taifa hili changa linaloanza kupiga hatua kuelekea kwenye maendeleo, usiogope kukosolewa kwa sababu hata hao wanaokukosoa nao hukosolewa pia-
Marcio Maximo wewe ni Bonge la Kocha lakini jua siku hazigandi.
Typed by:- Danny Msimamo a.k.a “Denyo”
Written by:- eric dizo aka dizo moko tupo pamoko watanzania!