Sambaza....

Huenda ukadhani masihara lakini kwenye soka kuna mambo mengi. Usione Mbwana Samatta yuko Genk, Ukadhani alifika kirahisi kuna misoto yake!

Cristiano Ronaldo, ni miongoni mwa wachezaji wenye mafanikio makubwa zaidi duniani, lakini hayo yote huenda yamechagizwa na rafiki yake kipenzi kipindi hicho anapambana mtaani kusaka timu ya kuichezea.

Ronaldo amekiri kuwa Albert Fantrau, ndiye rafiki yake mkubwa zaidi na wakaribu kipindi hicho aliyemsaidia kufikia malengo yake baada ya kusajiliwa na Sporting Lisbon akitokea timu ya mtaani ya Nacional da liha da Madeira.

Mambo yalikuwa hivi..”Tulikuwa tukicheza wote katika timu ya vijana, na siku moja mawakala wa Sporting Lisbon walitutembelea na kutuahidi kuwa, mchezaji atakayefunga magoli mengi zaidi ndiye atakayesaliwa kujiunga na Akademi ya klabu hiyo”

“Katika mechi hiyo tuiliibuka na ushindi wa goli 3-0, nilifunga goli la kwanza, na rafiki yangu Albert alifunga la pili, na goli la tatu ndilo goli lililowashangaza wengi, na mimi nikiwa  ni miongoni mwao..”

“Katika goli hilo, Albert alienda na mpira akiwa yeye na golikipa, na alifanikiwa kumpiga chenga golikipa na kubaki yeye na nyavu.. lakini cha kushangaza hakufunga goli na badala yake alitoa pasi kwangu ambaye nilikuwa nakimbia nyuma yake, nami bila ajizi nikafunga..”

“Baada ya mechi kumalizika, nilimfuata na kumuuliza kwanini alishindwa kupasia nyavu ziliyokuwa wazi na badala yake akatoa pasi kwangu! Naye akanijibu “Wewe ni bora kunizidi mimi”.. Ronaldo alisema.

Baada ya mechi hiyo, harakati za Albert kwenye soka ziliishia hapo, ndoto yake ilikuwa ni kumuona rafiki yake anapata nafasi anayostahili kuipata.

Licha ya kutokuwa na kazi, Albert anamiliki magali mazuri, nyumba na kumudu kuitunza familia yake. Albert amekiri kuwa hivyo vyote vinatoka kwa Ronaldo kama sehemu ya Shukrani yake.

Hadi sasa, Ronaldo ameweka na kuvunja rekodi nyingi katika ulimwengu wa Soka. Yote yalichangiwa na wema mdogo wa nusu dakika kutoka kwa rafiki yake Albert.  Albert amedhihirisha kuwa, wema hauozi,na kwa sasa anakula mafao yake kutoka kwa Ronaldo.

Umejifunza kitu? Toa maoni yako hapo chini..

Sambaza....