Sambaza....

Ni mwezi mmoja tuu ukiwa umabaki kuelekea kombe la dunia litakalofanyika June mwaka huu Urusi. Ligi zote  zikiwa zimekwisha macho ya wadau yakisubiri burudani kutoka kwa wachezaji wa mataifa 32.

Mwenyeji Urusi akitarajiwa kufungua dimba na Saudi Arabia ya michuano hiyo mikubwa kwa upande wa mpira wa miguu duniani.  Baadhi ya timu kama Argentina, Colombia, Costa Rica, Ujerumani zimeshaanza kutangaza vikosi vyao vya awali.

Kuelekea kombe la dunia kuna baadhi ya timu zimekua zikitajwa na kupewa nafasi kubwa kulinyakua kombe hilo. Timu kama Brazil, Argentina, Spain, Germany, Belgium na England zimekua zikipewa nafasi kuweza kubeba kombe hilo.

Kwa ubora wa vikosi vyao na wachezaji wanaounda timu zao nazipa nafasi timu hizi kuweza kufika nusu fainali ya kombe la dunia nchini Russia.!

Germany

Anakwenda Russia kama bingwa mtetezi baada ya kulichukua kombe hilo nchini Brazil kwa kuifunga Argentina katika dakika 120 kwa goli lá Mário Gotze.

Kikosi cha Ujerumani kinatarajiwa kuundwa na nyota kama Toni Kroose, Mesuit Ozil, Thomas Müller, Março Réus, Jerome Boateng na Ter Steven.

Chini ya kocha Joachim Low naipa nafasi kubwa Germany kuweza kufika nusu fainali na kuweza kutetea taji lake japo huenda akapata wakati mgumu akikutana na timu kama England na Argentina.

Wapo Kundi F: Germany, Mexico, Sweden, South Korea.

France

Mabingwa wa mwaka 1998 baada ya kuifunga Brazil mabao matatu kwa moja katika fainali zilizofanyika nchini kwao Ufaransa.

Kikosi cha Ufaransa kinategemewa kuundwa na mastar kama Paul Pogba, Antonio Griezman, Raphael Varane, Ngolo Kante, Bleise Matuidi na Kylian Mmbape. Huku ikipata pigo kwa kumkosa  beki wake tegemeo Konsielny alieumia akiwa na klabu ya Arsenal

Vijana wa Didier Deschaps mshindi wa kombe lá dunia mwaka 1998 akiwa kama mchezaji nakipa nafasi kubwa ya kurudia ya mwaka 1998 walipochukua ubingwa na 2006 walipofikiaa fainali na kufungwa na Italy kwa mikwaju ya matuta.

Wapo Kundi C: France،  Australia, Peru, Denmark.

Brazil

Mabingwa mara tano wa kombe lá dunia huku mara ya mwisho wakichukua kombe hilo mwaka 2002 Korea&Japan kwa kuifunga Ujerumani mabao mawili kwa sifuri, huku yote yalifungwa na Ronaldo De Lima.

Neymar Jnr, Fernandinho, Paulinho, Coutinho, Marcelo, Firmino, Casemiro na kipa wao Allison ni baadhi tuu ya nyota watakaovaaa jezi ya Brazil nchini Russia na kuweza kuirudisha tena Brazil kwenye ubabe na kutwaa tena kombe la dunia baada ya muda mrefu.

Tite kocha wa Brazil anategemea anatarajiwa kuipeleka timu yake njia salama mpaka kufika nusu fainali japo huenda akakutana na vigingi kama Ubeligiji, Colombia au Denmark.

Wapo Kundi E: Brazil, Switzerland, Costa Rica, Serbia.

Spain

Mabingwa pekee wa kombe la dunia katika ardhi ya Africa mwaka 2010 nchini Afrika Kusini. Walitwaa kombe hilo baada ya kuifunga Uholanzi katika dakika za nyongeza kwa goli la Iniesta.

Inaundwa na wakali kama Thiago Alcântara, Sérgio Busket, Andres Iniesta, Berelin, Gerald Pique na mlinda mlango bora duniani David De Gea. Ni baadhi ya nyota wanaotarajiwa kutandaza soka safi na kuipeleka Spain katika ndoto ya mwaka 2010.

Haitakua kazi rahisi kufika huko haswa kutokana na uwepo wa timu kama Ubeligiji, Mexico, Nigeria na Colombia.

Wapo Kundi B: Spain, Portugal, Morroco, Iran.

Sambaza....