Kocha wa timu ya Yanga Nesradeen Nabi amekutana na rungu la kamati ya masaa72 baada kumshushia adhabu kali ya kifungo pamoja na faini.
Katika mchezo wa kombe la FA kati ya Geita Gold na Yanga uliopigwa katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam Nabi alionyesha kadi nyekundu katika dakika za mwisho kutokana na kutoa lugha isiyostahiki kwa mwamuzi wa akiba.
Nabi amefungiwa mechi tatu pamoja na kutozwa faini ya 500,000, ambapo haruhusiwi kukaa kwenye benchi walaa kuingia katika katika vyumba vyakubadilishia nguo.
Miongoni mwa mechi atakazozikosa Nabi ni pamoja na mchezo wa Watani wa Jadi utakaopigwa April 30 katika mchezo ambao Yanga watakua mwenyeji. Katika mchezo wa raundi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Katika mchezo huo pia mlinzi mkongwe Kelvin Yondani ametozwa faini ya milioni moja na kufungiwa michezo mitatu kwa kosa la kumkanyanga Fiston Mayele.
Kelvin Yondani alimkanyaga makusudi Mayele ambae hakua na mpira ndani ya kumi na nane lakini hakuonwa na waamuzi. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja na baadae Yanga kushinda kwa mikwaju ya penati.