Sambaza....

Kuelekea mchezo wa fainali dhidi ya Azam Fc kocha wa Yanga amesema wanajisikia furaha kuelekea mchezo huo lakini alikiri ilikua ni ngumu kuwazuia Fiston Mayele na Aziz Ki wasiondoke klabuni hapo.

Yanga walitinga fainali baada ya kuwatoa Singida Big Stara fainali na kuelekea mchezo huo wa kesho Nabi amesema “Tunayo furaha kubwa kuwepo hapa kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Azam, tumefika leo lakini tutafanya kila jitihada kutetea ubingwa wetu tuliochukua msimu uliopita”

Nasradine Nabi pia alizungumzia kukosekana kwa Fiston Mayele na Aziz akisema ilikua ni ngumu kuwabakisha kutokana na majukumu ya timu zao za Taifa.

Fiston Mayele na Aziz Ki.

“Mayele na Aziz Ki wataokusa mchezo wa fainali kesho dhidi ya Azam kwasababu wameitwa kwenye majukumu ya timu zao za Taifa. Tarehe ya mchezo wa fainali wa kesho inaingiliana na tarehe za michezo ya timu za taifa lakini ilishindikana kubadilisha kwasababu ya changamoto za kiratiba.”

“Imefanyika jitihada kubwa kuwabakisha wachezaji wetu kwenye mchezo huu wa fainali lakini imekuwa ngumu kwa chama cha soka cha Congo na Burkina Faso kukubali maombi yetu kwa Mayele na Aziz Ki na kama Klabu tuna wajibu wa kuheshimu tarehe zilizopangwa na FIFA kwa wachezaji wetu kwenye majukumu ya kuwakilisha mataifa yao,” alisema kocha Nabi

Nahodha Bakari Nondo alikiri mchezo utakua mgumu kwao lakini wapo tayari na wamejiandaa kuwakabili Azam Fc fainali.

“Tunakwenda kukutana na timu ngumu kwenye mchezo wa kesho wa fainali lakini sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri kuwakabili Azam na kutetea ubingwa wetu,” alisema.

Sambaza....