Sambaza....

Yanga watashuka dimbani kesho usiku kuvaana na Simba katika fainali ya Ngao ya Hisani mkoani Tanga na tayari kocha wa Yanga ameonyesha kutokuwa na hofu na mchezo huo.

Gamondi aliyepokea timu kutoka kwa mtangulizi wake Nasraddine Nabi mwenye rekodi ya kuwafunga Simba katika michezo yote miwili ya Ngao ana kibarua kikubwa chakulinda rekodi hiyo.

 

Kocha huyo kuelekea mchezo huo alisema  “Ni Furaha kwangu kucheza derby kesho na haitakuwa na presha kwani nimeshakutana na derby nyingi hapo kabla,” alisema Gamondi na kuongeza;

“Hii siyo vita ni mpira wa miguu, ukishinda au kufungwa maisha yanaendelea kama kawaida.”

Sehemu ya bechi la ufundi la Yanga.

Gamondi aliyeiongoza Yanga katika michezo miwili dhidi ya Kaizer Chiefs na Azam Fc tayari ameonekana kuingiza falsafa zake na kuanza kushikwa na wachezaji wake.

Sambaza....