Kocha msadizi wa klabu ya Yanga Cedric Kaze ametoa maneno yake baada ya kuiongoza Yanga kupata ushindi mbele ya TP Mazembe tena wakiwa Lubumbashi katika uwanja wao wa nyumbani.
Cedrik Kaze ambae katika mchezo huo alisimama kama kocha kuu kutokana na Nasradine Nabi kutokuwepo hakusita kuwashukuru wachezaji wake na kuwamwagia sifa tele kutokana na walichokifanya Lubumbashi katika mchezo huo muhimu kwao.
“Pongezi kubwa kwa vijana wetu wameonyesha ukomavu katika mchezo mgumu katika mazingira magumu dhidi ya moja ya klabu kubwa (TP Mazembe) barani Afrika. Tunashukuru kwa sapoti kubwa ya mashabiki na uongozi wetu kwa ujumla, Wananchi furaha yenu ndio furaha yetu,” Cedrik Kaze alisema
Katika mchezo huo wa jana goli la Yanga lilifungwa na Farid Mussa aliyemalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango wa TP Mazembe baada ya krosi kutoka upande wa kulia kumshinda hivyo mpira kumkuta Farid akiwa pekeakee mbele ya lango.
Kwa ushidi huo sasa Yanga inaongoza kundi lake mbele ya US Monastir ya Tunisia huku ikiwaacha Real Bamako na TP Mazembe ikitolewa katika mashindano hayo. Wananchi sasa wanasubiri Aprili tano katika upangaji wa droo ili kumjua mpinzani wake.