Sambaza....

 

Mechi ya pili tangu ujio wa kocha mpya wa Simba Sven Vandenbroeck. Kocha ambaye alichukua nafasi ya Patrick Aussems. Mechi ya kwanza alicheza dhidi ya Arusha United na kushinda 6-0, na mechi ya pili ilikuwa dhidi ya Lipuli FC jana na akashinda 4-0. Ukitazama kuna ufanano wa ufundishaji Kati ya Sven Vandenbroeck na Pep Guardiola kwenye maeneo yafuatayo.

HIGH DEFENSIVE LINE.

Pep Guardiola mara nyingi huwa anawatumia mabeki wake wa Kati kuwa katika eneo ambalo viungo wa Kati wanatakiwa kuwa. Mabeki wa Manchester City mara nyingi huwa wanasogea mpaka katikati ya uwanja. Hiki kitu pia kipo ndani ya kikosi cha Simba kwa sasa.

Mabeki wa Kati wa Simba husimama katikati ya uwanja , na kuwalazimisha wapinzani wao muda mwingi wakae katika eneo Lao , hivo muda mwingi Simba inakuwa imeubana uwanja na inakuwa katika eneo la timu pinzani muda mwingi. Na mabeki hawa wa Kati ndiyo huanzisha mashambulizi , mfano pasi ya Pascal Wawa iliyozaa goli imetokea katikati ya uwanja eneo ambalo mabeki wa Kati wa Simba walikuwa wamejipanga.

INVERTED FULLBACKS

Wakati mabeki wa Kati wa Simba wanapokuwa wanasogea katikati ya uwanja , viungo wa Simba husogea mbele zaidi , mabeki wa pembeni wa Simba hujipenyeza katikati wakitokea pembeni kwa ajili ya kuziba maeneo ambayo yameachwa wazi na viungo wa Kati ambao mara nyingi husogea mbele.

Kapombe

COUNTER PRESSING

Mara nyingi Pep Guardiola ana kanuni moja , kipindi ambacho timu inapoteza mpira , huwa anaipa timu yake mtihani wa kuurudiaha ndani ya sekunde 30, hiki ndicho kitu ambacho kinaonekana kwa Simba katika mechi hizi mbili , Simba ikipoteza mpira hufanya pressing haraka ili kuurudisha, kocha Sven Vandenbroeck anaonekana anataka kila muda timu yake iwe na mpira kama ilivyo kwa Pep Guardiola .

Sambaza....