Sambaza....

Kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba dhidi ya wenyeji wao Raja Casablanca kocha wa Simba Robert Oliveira amesema wamejiandaa kupata ushindi mbele ya wenyeji wao.

Simba itashuka Dimbani Ijumaa saa nne usiku kwa saa za Morocco sawa na saa saba usiku kwa Tanzania kukabiliana na vigogo wa Afrika Raja Casablanca katika dimba la Mohamed V kucheza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.

 

Akizungumza mbele ya Waandishi wa habari kuelekea mchezo huo Robert Oliveira ametoa ahadi ya ushindi kutokana na maandalizi mazuri waliyokua nayo wiki yote hii.

“Nimeiandaa vizuri timu yangu kwaajili ya mchezo huu. Malengo yangu ni kucheza vizuri na kushinda,” alisema Robertinho

Nae mkongwe Saidoo Ntibazonkiza akiongea kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema wamechoka nafari lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya wao kutoka na matokeo mabovu katika mchezo huo wa ugenini.

Kiungo mshambuliaji wa Simba Saidoo Ntibazonkiza (katikati) akiwatoka wachezaji wa Vipers katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Saidoo Ntibazonkiza “Tumejiandaa vizuri japo bado tuna uchovu wa safari lakini kwetu haitakua sababu. Kama wachezaji tunajua kazi yetu. Tutahitaji kufanya vizuri iwezekanavyo.”

Simba watakua wageni wa Raja ambao nawao ni kama Simba wameshafuzu kwenda robo fainali ya michuano hiyo. Katika msimu uliomalizika wa Ligi ya Mabingwa Afrika Raja Casablanca waliishia nusu fainali.

Sambaza....