Sambaza....

Kuelekea mchezo wa Watani wa Jadi makocha na manahodha wa klabu ya Simba wameongea mbele ya waandishi wa habari huku wakijinasibu kuondoka na alama zote tatu katika mchezo ambao wao ndio watakua wenyeji wa mchezo.

Kuelekea mchezo huo kocha mkuu wa klabu ya Simba Robert Oliveira amesema wala hana hofu na mchezo huo kwani hawaiogopi Yanga na amewataka mashabiki waje kwa wingi kushuhudia kandanda safi katika dimba la Benjamin Mkapa.

 

“Bado nasisitza siuhofii mchezo huu dhidi ya Yanga, tunakwenda kutafuta ushindi muhimu kwa timu yetu. Natamani kuona uwanja ukiwa umejaa ili watu washuhudie kandanda safi hapo kesho kwani Simba tupo tayari kwa mchezo na nimewaandaa wachezaji wangu kushinda mchezo,” alisema Robertinho.

Kocha huyo Mbrazil amesema kwa upande wake kandanda ni sanaa na burudani hivyo anapenda kuwaburudisha mashabiki kiwanjani akiwa na wachezaji wake bora.

Robert Oliveira “Lengo letu ni kuhakikisha tunashinda kila mechi na kucheza vizuri. Nawajua vizuri wapinzani wetu Yanga, tunawaheshimu lakini tumejipanga. Mpira kwangu ni sanaa na napenda wachezaji wacheze na kuwafurahisha mashabiki pia.” 

Simba atakua nyumbani kesho katika Dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 11 jioni, mpaka sasa wanakutana tayari Yanga ni kinara akimuacha alama nane Simba katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Sambaza....