Leo klabu ya Simba imemtangaza Pierre Lechantre kuwa kocha mkuu wa Simba akisaidizana na Masoud Djuma ambaye alichukua ana kaimu nafasi iliyoachwa wazi na kocha Joseph Omong.
Pierre Lenchantre ni kocha mwenye elimu kubwa ya ukocha akiwa na cheti cha UEFA pro licence, cheti cha ngazi ya juu kabisa ya ukocha barani Ulaya.
Cheti ambacho kinampa nafasi kocha huyo kufundisha timu inayoshiriki UEFA ( klabu bingwa ulaya) na ligi yoyote kubwa barani ulaya kama ligi kuu ya England.
Aliwahi kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001, ambapo aliisaidia timu ya Taifa ya Cameroon kushinda kombe la Afcon mwaka 2000.
Alizaliwa miaka 67 iliyopita nchini Ufaransa. Ambapo kabla ya kuwa kocha amewahi kuwa mchezaji katika timu mbalimbali kama Paris Fc, Red Star 93,Stade de Reims, Olympique De Marseile, RC Lens,Stade Lavallois, As Monaco, FC Sochaux,Lille OSC.
Pamoja na kwamba aliwahi kuifundisha timu ya taifa ya Cameroon , katika Afrika aliwahi kuzifundishi timu za Al-Ittihad Club (Libya), CS Sfaxien (Tunisia) ana Club Africain (Tunisia).
Amekuwa kocha ambaye hadumu kwa muda mrefu na timu moja, hajawahi kukaa na klabu ya Afrika ndani ya mwaka mmoja.
May 2012 alichaguliwa kuifundisha timu ya taifa ya Senegal , lakini wiki moja baadaye baada ya uteuzi wake alitangaza kuacha kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Senegal baada ya kutokufikia makubaliano na shirikisho la soka nchini Senegal FSF.
January 13 mwaka 2016 timu ya taifa ya Congo Brazzavile ilimchukua awe kocha mkuu wa timu ya taifa na aliikuta timu ya Taifa ikiwa inaongoza kundi katika mechi za kufuzu Afcon 2017 kwa tofauti ya magoli na timu ya Taifa ya Zambia, lakini mwisho wa siku hakuiwezesha timu kufuzu, na timu iliyofuzu katika kundi lao ilikuwa Guinnea-Bissau.
Katika harakati za kufuzu kombe la dunia nchini Russia (2018) Congo Brazzavile ilifungwa mchezo dhidi ya Misri baada ikafungwa goli moja dhidi ya Uganda na ikawa mechi ya mwisho kwake, shirikisho la soka la Congo Brazzavile lilivunja mkataba wake.
Siyo jambo la kawaida kwa kocha huyu kufukuzwa kwani aliwahi kufukuzwa baada ya mechi tatu akiwa na timu ya Al Arabi ya nchini Qatar, hii baada ya kutoka sare michezo miwili na kupoteza mmoja.