Sambaza....

Kocha mkuu wa Al Ahly Pitso Mosimane ameonekana kutilia shaka kwa nchi ya Morroco kuchaguliwa mwenyeji wa Fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF jana lilitangaza nchi ya Morocco itakua mwenyeji wa fainali za Ligi ya Mabingwa msimu huu, huku nchi nne zikiwa na washiriki katika nusu fainali na Morroco ikiwepo.

Miongoni mwa timu zinazoonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kutinga fainali ni Wydad Casablanca na Al-Ahly. Katika michezo ya kwanza ya nusu fainali Al Ahly walimfunga ES Setif mabao manne kwa bila, wakati Wydad wao walishinda mabao matatu kwa moja dhidi ya Petro Luanda.

Hivyo kitendo cha CAF kuichagua Morocco kama mwenyeji wa fainali hizo ni kama kupa faida Wydad endapo watatinga fainali kwani watakua wanacheza nyumbani.

Mshambuliaji wa Wydad Casablanca akishangilia katika mchezo dhidi ya Petro Luanda

“Wakati michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilipokamilika, fununu zilikuwa zikisema SA ni mwenyeji,” Pitso Mosimane

Mosimane aliongeza “Hao, jikijiki, baada ya michezo ya nusu fainali kuamuliwa, palitokea ukimya mkubwa nchi ya kuandaa fainali.  Kisha baada ya mkondo wa kwanza wa nusu fainali, ghafla Morocco ni mwenyeji.” Alimalizia kocha huyo kutoka Afrika Kusini.

Percy Tau wa Al Ahly akimtoma mlinzi wa ES Setif.

Endapo Ahly watafuzu fainali watakua wameingia fainali ya kombe hilo mara tatu mfululizo na kama wakitwaa kombe hilo watakua wamelibeba mara tatu mfululizo.

Sambaza....