Sambaza....

Kikosi cha KMC FC kesho kitashuka katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa saa kumi jioni huku ikiendelea kumkosa kiungo wake fundi Baraka Majogoro.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana itawakaribisha Kagera Sugar ya mkoani Kagera ambapo pamoja na mambo mengine mipango na mikakati ya maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa asilimia kubwa.

 

Kocha Msaidizi Ahmad Ally amesema kuwa kama benchi la ufundi limefanya maandalizi ya kutosha na kwamba kila mmoja yupo tayari katika mchezo huo na kusisitiza kuwa utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kwamba Kagera Sugar inushindani kwani hata kwenye msimamo wa Ligi wapo kwenye nafasi nzuri.

Ahmad ameongeza kuwa katika mchezo wa kesho kama Timu inahitaji matokeo mazuri kutokana na kwamba KMC FC hapo kwenye nafasi nzuri na hivyo kuhitaji zaidi ushindi ili kutoka kwenye nafasi hiyo na hivyo kujiimarisha kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Baraka Majogoro

” Tunakwenda kucheza nyumbani lakini tutakuwa na mechi ngumu kwa kuwa tunapresha ya kukosa matokeo rafiki kwenye michezo yetu iliyopita, Ila tumejipanga kukabiliana na presha hiyo lakini pia kutumia vizuri uwanja wa nyumbani ” amesema Kocha Ahmad.

Kuhusu Afya za wachezaji, Kocha Ahmad amesema kuwa wote wapo kwenye hali na morali nzuri na kwamba tutamkosa mchezaji mmoja ambaye ni Baraka Majogoro kutokana na sababu za majeraha huku Kelvin Kijiri na David Kisu Mapigano ambao walikuwa na changamoto hiyo wamesharejea kikosini.

 

 

Kevin Kijiri “Kevin Nash” akiwa na Ally Ramadhani “Oviedo”

Katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya NBC KMC FC ilipoteza ugenini dhidi ya Azam kwa goli moja kwa sifuri mchezo ambao ulipigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi na kwamba katika msimamo ipo nafasi ya 13 ikiwa imekusanya jumla ya alama 23 na kucheza michezo 24.

Sambaza....