Sambaza....

Baada ya mchezo wa kanda ya ziwa dhidi ya Mwadui FC na kutoka sare ya bao 1-1, timu ya soka ya Manispaa ya Kinondoni ‘KMC’ imerejea Jijini Dar es Salaam ambapo Leo Imeanza Mazoezi rasmi ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Azam FC.

Kocha msaidizi wa KMC Ahmad Ally amesema maandalizi ya kuelekea mchezo huo yanaendelea Vizuri na kwamba kutokuwapo kwa Juma Kaseja kwenye kikosi hakutaathiri maandalizi ya mchezo huo kwani Bado wanakikosi kipana.

Amesema Juma ambaye amejiunga na timu ya Taifa ya soka la Ufukweni kwa ajili ya mechi za Mataifa Afrika nchini Misri hatokuwa sababu kwa timu hiyo kutopata alama tatu dhidi ya Azam FC.

“Huwezi kusema kwamba kukosekana kwa Juma kutaathiri, ukijaribu kuangalia wakati alipokuwepo Kuna mechi alitumika na Kuna mechi hakutumika, lakini tulifanya Vizuri tu, tunajua pia yule ni nahodha lakini Kutakuwa na nahodha mwingine, kutokuwepo kwake ni moja ya kazi yake kwa maana ameitwa akawajibike kwenye timu ya Taifa, tumesajili wachezaji zaidi ya 28, ni muhimu kujua Baada ya Juma kuna mbadala wake tena ni kipa ambaye anacheza timu ya Taifa ya Burundi,” Ahmad amesema.

Vile vile Ahmad akagusia suala la usajili ambapo amesema kuwa Bado wanaendelea na zoezi Hilo lakini kwa sasa hawawezi kuzungumza chochote hadi pale mchezo dhidi ya Azam utakapokamilika.

KMC inayoongozwa na Kocha wa zamani wa Mbao FC Ettiene Ndayiragije wanashika nafasi ya 11 wakiwa na alama 17, wakishinda michezo mitatu pekee kati ya michezo 14 ambayo wamecheza mpaka hivi sasa.

Sambaza....