Sambaza....

Baada ya michuano ya Ulaya (UEFA&EUROPA League) kuhitimisha hatua ya 16 bora hapo jana imeonekana klabu za Ligi Kuu Uingezereza kuwatesa wenzao wa Ulaya katika kufuzu hatua ya robo fainali.

Katika michuano hiyo mikubwa barani Ulaya Ligi Kuu Uingereza imetoa timu 6 zilizofuzu kucheza robo fainali na hivyo kuandika historia mpya kwa Taifa hilo. Mara ya mwisho nchi hiyo kufanya hivyo ni mwanzoni mwa miaka ya 1970.

Timu hizo ni nne katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ambazo ni Manchester United, Manchester City, Liverpool na Totenham Hotspurs. Lakini pia hii imetokea baada ya miaka 10 kupita.
Pia katika Europa League kuna Chelsea na Arsena. Hivyo kufanya kufikisha idadi ya timu sita katika michuano ya Ulaya.

Sambaza....