Kiungo wa klabu ya Yanga Mudathiri Yahya Abas ameibuka kinara mbele ya wachezaji wengine Afrika baada ya bao lake kuchaguliwa kuwa bao bora la hatua ya makundi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Goli la Mudhathir alilofunga dhidi ya TP Mazembe katika mchezo uliopigwa Benjamin Mkapa ambapo ulikua mchezo wa wiki ya pili wa Kombe la Shirikisho Afrika ndilo lililopigiwa kura nyingi na kuibuka kinara. Katika mchezo huo Yanga waliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja.
Kiungo huyo wa Yanga aliibuka kinara kwa kupata kura 71% mbele ya Aymen Mahious 21% [USM Algier], Aubin Kouame 5% [Asec Mimosa] na Paul Acquah 3% wa Rivers United.
Mudathir alijiunga na Yanga katika dirisha dogo akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Azam Fc. Mpaka sasa katika michezo yote Mudathir aliyohusika katika michuano ya Shirikisho amefunga bao moja pekee.
Kiungo huo wa Taifa Stars baada ya kuiongoza Yanga kuvuka makundi na kwenda robo fainali sasa wanatarajiwa kucheza na kati ya Pyramida, USM Algier au Rivers United