Mchezaji wa timu ya KMC “Kino Boys” na timu ya Taifa U-20 Ngorongoro Heroes Ally Msengi huenda akaelekea katika moja ya klabu ya Ligi Kuu nchini Afrika ya Kusini.
Baada ya kuonyesha mchezo wa kuvutia tangu alipoiwakilisha timu ya Taifa ya chini ya miaka 17 Serengeti Boys katika michuano nchini Gabon ameonekana kuvivutia vilabu kabdaa vya nje ya nchi na hivyo kupelekea kualikwa kwenye majaribio katika nchi kadhaa barani Afrika.
Tovuti ya Kandanda baada ya kupata tetesi hizo tulifanya juhudi ya kupata ukweli wa hili na ndipo tulipomtafuta msemaji wa KMC Anuary Binde ili kutupa ukweli wa habari hizi.
Anuary Binde “Hizo ni tetesi tuu na bado hazijawa official, kila kitu kikiwa official tutatoa taarifa kwenu. Kwasasa hizo zinaendelea kua tetesi tuu, na mchezaji mwenyewe yupo mazoezini hapa na kesho huenda akacheza katika mchezo wetu dhidi ya Simba.”
Klabu ya Stellenbos inayoshirki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini ndio inatajwa kutaka saini ya kiungo huyo mkabaji wa KMC. Stellenbos ipo nafasi ya 13 ikiwa na alama 15 huku ikicheza michezo 15 mpaka sasa.
Kama atafanikiwa kujiuna nao maana yake atakwenda kukutana na kaka yake Abdi Banda anaecheza katika klabu ya Highland Park nchini humo.