Sambaza....

Kiungo aliyeitumikia Azam Fc kwa misimu miwili Keneth Muguna amekiri ubora wa Ligi ya Ligi Kuu bara na kusema ni bora kuliko ligi ya kwao Kenya kwasasa.

Muguna ambae yupo kwao Kenya baada ya Ligi kumalizika na kuachana na Azam Fc baada ya mkataba wake kumalizika alisema “Kwa sasa Ligi ya Tanzania ina ushindani mkubwa kuliko Ligi Kuu ya Kenya. Kenya Ligi imekuwa ikisimama kwa mwaka mmoja au zaidi (kwa sababu ya kusimamishwa kwa FIFA),” Muguna aliambia kipindi cha redio nchini humo na kuongeza “Hii (kusimamishwa) iliathiri ligi ya Kenya na kuiangusha ligi na timu ya taifa kwa sababu tulikuwa hatuchezi.”

Nyota huyo wa zamani wa Western Stima aliongeza pia mashindano ya CAF Sababu nyingine inayoifanya kuhisi logi ya Tanzania ni bora zaidi ni jinsi Simba na Yanga SC zimekuwa zikifanya vyema katika mashindano ya CAF.

Keneth Muguna.

Simba imekuwa ikishiriki Ligi ya Mabingwa mara kwa mara, huku Yanga ikiwa imetinga fainali msimu huu kwenye Kombe la Shirikisho. Walifungwa na USM Alger ya Algeria katika fainali za mikondo miwili zilizochezwa Tanzania na Algeria.

“Hata ukiangalia mwenendo wa timu za nchi zote mbili kwenye michezo ya Afrika, na hata kuangalia jinsi ligi za Tanzania zinavyopangwa, ni juu zaidi ya za Kenya. Ligi ya Tanzania inavutia sana, na kila mmoja anataka kwenda kucheza huko,” aliongeza.

Keneth Muguna alijiunga na Azam Fc akitokea Gor Mahia ya Kenya ambapo alikaa Chamanzi miaka miwili. Kwasasa ni mchezaji huru na yupo kwao Kenya kwa mapumziko.

Sambaza....