Sambaza....

Mnamo tarehe 3 Machi 2001, Bayern Munich ilikuwa nyuma kwa goli 3-2 dhidi ya Hansa Rostock kwenye mechi ya ligi kuu Ujerumani maarufu kama Bundesliga, kabla hawajapata kona katika dakika za lala salama.

Golikipa Oliver Kahn alipanda kwenda kushambulia, ilipopigwa kona aliruka juu na kuupiga mpira kwa mikono na ukatinga ndani ya nyavu.

Mwamuzi wa mchezo huo mtaalamu wa kipenga Merkus Merk akampa kadi nyekundu na Bayern ikapoteza mechi hiyo.

Oliver Khan (jezi namba 1) akionyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi.

Baadaye Kahn akatania kuhusu tukio hilo, kwa kusema; alidhani kuwa golikipa anaruhusiwa kutumia mikono ndani ya box.

Kweli hapo Kahn alitania kwa sababu kanuni ipo wazi kabisaaa! Golikipa anatakiwa kudaka ndani ya box lake tu, nje ya hapo anakula kadi nyekundu bila kuuliza!


Sambaza....