Sambaza....

Wiki iliyopita ilikuwa wiki ngumu sana kwa Pep Guardiola baada ya kupoteza michezo miwili kwa magoli sita (6) jumla, kazi kubwa waliyonayo leo ni wao kuhakikisha wanaifunga Liverpool kuanzia magoli 4-0 ili wafanikiwe kufuzu kwenda hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

Manchester City wanaweza kufunga magoli bila kuruhusu goli?


Hiki kitu ni kigumu sana kwao kwa sababu hata ukiangalia katika mechi mbili zilizopita ameruhusu magoli sita (6) ameruhusu na timu za aina gani? Hapa ndipo ugumu wa Manchester City kumaliza mchezo bila kufungwa leo.

Aina ya timu ambazo amekutana nazo katika mechi mbili zilizopita ni timu ambazo zinakabia kwa juu (zina press high) ndiyo maana zilifanikiwa kupata goli dhidi ya Manchester City.

Manchester City inaweza ikaonekana kama timu ambayo haijaruhusu magoli mengi. Lakini kiurahisia Manchester City aina yao ya uchezaji huwafanya wasiruhusu kushambuliwa sana. Muda mwingi timu hukaa mbele ya mpira na hii huwafanya wasiruhusu magoli mengi na kuficha udhaifu wao unaoonekana wakati wanajizuia.

Manchester City hutengeneza uwazi mkubwa sana wanapokuwa wanajiuzia. Uwazi ambao husababisha timu pinzani kutumia na kufunga. Timu ambazo zimefanikiwa kupata goli dhidi ya Manchester City zilitumia uwazi uliokuwa unatengenezwa na mabeki wa Mnachester City huko nyuma.

Pili, Manchester City inapokabiwa juu mabeki wake hulazimishwa kufanya makosa ambayo huadhibiwa.

Liverpool ina wachezaji wa mbele ambao hukabia juu kwa kasi, mechi zote mbili ambazo wamechezaji Anfield dhidi ya Manchester City, waliwalazimisha mabeki wa Manchester City wafanye makosa binafsi kutokana na wao kukabia juu.

Jurgen Klopp, Meneja wa Liverpool.

Hiki ni kitu cha pili ambacho kinatia ugumu kwa Manchester City kumaliza mechi bila kuruhusu goli.

Kitu cha tatu na cha mwisho, ni safu ya ushambuliaji ya Liverpool ambayo kwa msimu huu wa ligi ya mabingwa barani ulaya ndiyo safu ambayo imefunga magoli mengi katika michuano hii ya Ulaya kuzidi timu zote zinazoshiriki Michuano hii.

Magoli ishirini na nane (28) katika michezo tisa (9) ikiwa ni wastani wa kufunga magoli matatu (3) katika kila mechi kwenye msimu huu wa ligi ya mabingwa barani ulaya, hii inatoa mwanga kuwa Liverpool hawezi kumaliza mechi bila kufunga goli.

Ubora wa safu ya Ushambuliaji ya Manchester City unatoa tafasri gani kwenye hii mechi ya leo?


Kuna tafasri moja inayokuja baada ya kutazama safu ya ushambuliaji ya Manchester City na safu ya ushambuliaji ya Liverpool. Hizi ndizo safu Imara za ushambuliaji pale kwenye ligi kuu ya England zilizofunga magoli mengi.

Hii inatosha kuonesha kabisa timu hizi katika mechi ya leo zitafungana, na idadi kubwa ya magoli yanaweza kupatikana.

Image result for liverpool vs man city uefa champions league

Kipi wakifanye Manchester City ili wavuke?


Kitu cha Muhimu ni Pep Guardiola kujidhatiti kwanza katika eneo la kujilinda. Leo lazima aende kushambulia lakini anatakiwa kumpa heshima Liverpool kwa kushambulia kwa tahadhari ili wasiruhusu goli.Safu ya ulinzi inatakiwa kuwa imara zaidi kwa sababu safu ya ushambuliaji ni bora na ina uwezo wa kufunga magoli.

Kipi wakifanye Liverpool ili wafanikiwe kupita?


Wakubali kuwa underdog(s) kwenye hii mechi, ukikubali kuwa underdog(s) unakuwa na uwezo wa kumheshimu mpinzani wako na kuna kuwa na nidhamu ya matumizi ya kila nafasi wanayotumia pia umakini kuongezeka ndani yao , umakini ambao utawafanya wawe makini sana wanapojilinda kutokufanya makosa mengi binafsi

Sambaza....