Kikosi cha Yanga kimeondoka leo asubuhi kulekea nchini Congo kwenda kuivaa TP Mazembe katika mchezo wa mwisho wa Kundi D katka Kombe la Shirikisho Afrika. Mchezo hio utapigwa siku ya Jumapili jijini Lubumbashi.
Wakiwa uwanja wa ndege kuelekea nchini Congo Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema wamejiandaa vyema kuelekea mchezi huo na wanakwenda Congo ili kuendeleza walipoishia.
“Tunaondoka leo na kama mnavyojua wachezaji wengi walikua timu zao za Taifa hivyo wengine tutakutana nao kule, tutafika Lubumbashi saa saba mchana. Wachezaji waliobaki nadhani mlikua mnaona kupitia mitandao ya kijamii walikua wanaendelea na mazoezi kule Avic kwaajili ya kujiandaa na mchezo huu dhidi ya majirani zetu Tp Mazembe. Tunakwenda kumalizia pale tuliopishia katika mchezo wa mwisho hapa Dar,” alisema Arafat Haji.
Yanga wanakwenda kucheza mchezo dhidi ya Tp Mazembe wakiwa kileleni mwa kundi hilo wakiwa na alama 10 sawa na US Monastir wakiwaacha Mazembe na Bamako nafasi ya tatu na nne.
Kupitia mchezo huo Arafat Haji amesema wanauchukua mchezo wa muhimu kwani wanataka kuionyesha Afrika Yanga ni timu ya aina gani na hawataki kupoteza uongozi wa kundi lao.
Arafat Haji “Lengi letu ni kutuma ujumbe kwamba Yanga imejiandaa na michuano hii ya Afrika kupitia mchezo huu dhidi ya Mazembe, kama ambavyo tunaondoka leo tunaongoza kundi basi pia tunataka tukirudi Jumatatu hapa tuwe bado kileleni mwa kundi letu.”
Yanga tayari wameshafuzu kwenda robo fainali ya michuano hiyo yapili kwa ukubwa Afrika katika ngazi za vilabu na wanachokwenda kufanya Congo ni kutafuta uongozi wa kundi ili kupata faidi ya kuanzia ugenini katika robo fainali.