Sambaza....

Msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ali amezungumza baada ya kutolewa kwa timu na kumesema timu yao haijakwenda mbele wala kurudi nyuma. Simba imetolewa katika hatua ya Robo fainali ya Kombe la Shirikisho na Orlando Pirates kwa mikwaju ya penati.

“Kwenye maisha ni muhimu kupia hatua kwenda mbele, kama haupigi hatua kwenda mbele basi usipige hatua kurudi nyuma.
Simba hatujapiga hatua kwenda mbele lakini uzuri hatujapiga hatua kurudi nyuma pia.” Alisema Ahmed Alli



“Msimu wa tatu tunaishia robo fainali inaumiza lakini kwa upande mwingine inatia matumaini na faraja kwamba tunamaintain ubora wetu.
Kwa jicho la maendeleo kuna improvement kubwa kwenye timu yetu na uzuri ni kwamba tunajifunza kila msimu unapoisha. ” Anaongeza Ahmed msemaji wa klabu ya Simba.

Pia Ahmed Ali hakusita kuwapa pole mashabiki wa Simba kwa kipigo hicho lakini pia akiwapa neno la matumaini na kuwahakikishia ubora wa timu yao katika ukanda huu.

Sadio Kanoute (13) “Mkuki” akiruka juu kugombea mpira na mchezaji wa Orlando Pirates.

“Poleni sana Wanasimba wenzangu, msikatishwe tamaa na watu wasiojua hata makundi yanafananaje.
Sisi ni bora sana katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuitawala Afrika ni swala la muda tuu.” Ahmed Alli

Simba kwa mara ya tatu inashindwa kuvuka hatua ya robo fainali katika michuaono ya Afrika. Awali ilitolewa na TP Mazembe msimu wa 2018/2019, halafu ukatokewa msimu uliopita na Kazier Chiefs na sasa imetolewa na Orlando Pirates.

Sambaza....