Sambaza....

Simba leo imefanya mazoezi yake ya mwisho leo jioni katika uwanja wa Bokko Beach Veteran kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya TP-Mazembe kesho saa kumi jioni katika uwanja wa Taifa “Kwa Mkapa” jijini Dar es salaam.

Katika mazoezi hayo yaliyoanza saa kumi kamili jioni yakisimamiwa na makocha wote wa Simba na meneja Rweyemamu huku wakikosekana daktari Gembe wa timu na mtunza vifaa Mdundo Mtambo na mratibu Abass Ally waliokua wakishughulikia mambo mengine kwaajili ya mchezo wa kesho.

Baada ya kupasha misuli na mwalimu wa Simba alivigawa vikosi viwili huku timu moja ikiwa imevaa bips za CAF na wengine wakiwa hawajavaa bips.
Katika kikosi kilichovaa bips ambacho huenda kikaanza kesho kilikua na kipa Aishi Manula, Coulibaly, Mohamed Hussein, Wawa, Nyoni, Kotei, Niyonzima, Mkude, Kagere, Bocco na Chama.
Ambapo kikosi cha pili kilikua na kipa Deo Dida, Gyan, Kwasi, Juuko, Bukaba, Mo Ibra, Dilunga, Mzamiru, Mo Rashid, Salamba na Okwi.

Niyonzima na Chama pamoja

Katika mazoezi hayo baada ya mwalimu kupanga vikosi viwili huku Chama na Niyomzima wakiwa pamoja walicheza kwa kuelewana sana kiasi cha mashabiki nje wakitamani kesho waanze pamoja. Kwa mujibu wa mwalimu huenda kesho mafundi hawa wakaanza katika kikosi cha kwanza dhidi ya Mazembe.

Haruna Niyonzima na Cleotus Chama

Hata baada ya mazoezi kuisha wawili hao walionekana wakiwa pamoja kama wanajadili mambo huku wakionekana wenye hamasa.

 

Sambaza....