Ligi ya klabu bingwa barani Africa imemaliza hatua ya awali na sasa inaingia mzunguko wa kwanza ambapo utapigwa tena katika ya December 14 na 16 na michezo ya marudiano utapigwa kati ya December 22 na 24.
Wachezaji wawili wa kimataifa katika vilabu vya Nkana Rangers ya Zambia na Simba sc ya Tanzania zitakutana katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo na kuwafanya wachezaji wake muhimu kurudi nyumbani.
Hassan kessy anaechezea katika klabu yake mpya ya Nkana red devils aliyojiunga nayo msimu huu akitoka Yanga atakua na kibarua kigumu dhidi ya Simba Sc ambao ni waajiri wake wa zamani.
Hassan kessy alijiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar na kukaa kwa msimu mmoja na nusu kabla ya kuhamia kwa mahasimu wao Yanga. Hivyo katika mchezo wa marudiano utakaopigwa December 24 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam utakua umemrudisha nyumbani mlinzi huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania.
Cletus Chama yeye atakua na wakati mzuri atakapokua amerudi nchini kwao Zambia alipotoka huko msimu uliopita alipokua akiitumikia klabu ya Lusaka Dynamos. Katika mchezo wa kwanza utakaopigwa December 14 nchini Zambia Chota Chama atakua na jezi ya Simba huku akiwa mchezaji wa kutumainiwa kwa wekundu wa msimbazi.
Ikumbukwe Simba sc imefika hatua hii baada ya kuiondosha klabu ya Mbabane Swallows kwa jumla ya mabao nane kwa moja.
Nkana Rangers wao waliitoa Ud Songo kwa ushindi wa jumla ya mabao matatu kwa moja.