Sambaza....

Nyota wa Juventus, Christiano Ronaldo amesema anatarajia kuwa huru hivi karibuni kutokana na kesi ya ubakaji inayomkabili.

Ronaldo ambaye amethibitisha kujiamini kutokana na kesi inayomkabili, mwenyewe akiita “shambuli la kingono”  dhidi ya mwanamitindo Kathryn Mayorga, mwaka 2009, Las Vegas nchini Marekani.

Ronaldo ambaye alikaa kimya tangu habari za kushtakiwa kwa kosa la ubakaji ziliposambaa katika vyombo vya habari, leo akiwa nchi kwao Ureno, uzalendo umemshinda na kuamua kufunguka juu ya kesi hiyo.

“ naumia sana kuona familia yangu inazipata habari hizi zenye kuumiza,  japo wananijua kuwa siwezi nikafanya hivyo”

“ nimetulia na najiamini , mambo yatakuwa vizuri hivi karibuni” aliongea nyota huyo wa zamani wa Man U na Real Madrid.

Mwanamitindo Kathryn Mayorga alifungua kesi ya ubakaji dhidi ya Ronaldo mwezi septemba mwaka 2018. Polisi wa Las Vegas wamethibitisha kuwa ni kweli kuna jarada la uchunguzi lililofunguliwa juu ya mashtaka ya mwanamitindo huyo kwa Cr7.

Mwezi Oktoba mwaka jana, ikiwa ni mwezi mmoja tangu, taarifa za kesi ya ubakaji kuenea kwenye vyombo vya habari duniani , Ronaldo alitumia ukurasa wake wa Twitwer, kuandika maneno yenye kuonesha kushangazwa na taarifa hizo.

“ nayakataa madai hayo, nakataa nikijiamini kabisa, ubakaji ni uharifu usio wa kawaida, unaopingana na kila kitu, ni kinyume na falsafa za maisha yangu kama Ronaldo, hivyo siwezi kuutenda uharifu huo”.

Mayorga ambaye alivitaarifu vyombo vya habari kuwa, Ronaldo mwenye thamani ya paundi milioni 100 yupo tayari kumpa pesa ili asizitoe taarifa hizo, lakini Ronaldo kwa upande wake anaziita kuwa ni “ habari za kuzusha”.

Kitendo cha ubakaji kinadaiwa kutokea mapema juni 13, mwaka 2009, kipindi hicho Ronaldo akiwa na miaka 24 pekee, wakati mwana ndinga huyo akiwa mapumzikoni nchini Marekani, na shemeji yake pamoja na binamu yake.

Kipindi hicho Kathryn Mayorga, alikuwa akifanya kazi katika baa moja inayofahamika kwa jina la  Rain Nightclub, mwadada huyo alikutana na Ronaldo katika sehemu ya watu wa daraja la juu “VIP” na huko ndiko mambo yote yalitokea likiwemo la  kumbaka mwanadada huyo ambaye kipindi hicho mwaka 2009 alikuwa na miaka 25.

Ripoti zinadai kuwa, Ronaldo alikubali kumlipa mwanamitindo huyo hadi dola za kimarekani 287,000 ili kuzuia madai yake kufika mahakamani lakini juhudi zake ziligonga mwamba.

Endapo Ronaldo atakutwa na hatia, adhabu yake bila shaka ni kifungo cha maisha jela. Polisi wa Las vegas wamedhamilia kumuhoji Ronaldo juu ya kile kinachomkabili.

 Mseamji wa polisi amesema kuwa wao kama polisi hawajui watamuhoji lini Ronaldo lakini lazima wamuhoji, ili kusikia chochote kutoka kwake.

Sambaza....